OCD Galiyamoshi ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mashindano hayo akiongea na wachezaji na mashabiki kabla ya kukabidhi zawadi ya mbunzi kwa washindi
Mmoja wa wasimamizi wa mashindano Bw.Jerome Bange akisoma taarifa ya mashindano kwa mgeni rasmi
Kamanda wa TAKUKURU Edings Mwakambonja akiongea na wachezaji pamoja na mashabiki wa pambano hilo
Muandaaji wa mashindano hayo kulia Mh.Lukuna akiwa na wageni waalikwa pamoja na wadhamini wa mashindano hayo
vijana wa timu ya Town stars wakiwa na furaha baada ya kushinda
Waamuzi wakimsikiliza mgeni rasmi
Mgeni Rasmi akimkabidhi Mbuzi kongozi wa timu ya Town stars
Wachezaji wa timu ya Town stars wakifurahi kwa kumnyanyua Mbuzi juu baada ya kukabidhiwa
Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Edings Mwakambonja akiwa na washindi wa mashindano hayo yimu ya Town Stars katika picha ya pamoja
TIMU ya mpira wa miguu yenye makao yake
makuu Ludewa mjini ijulikanayo kama Town Stars imeibuka kidedea baada
ya kuichapa magli 3 kwa bila timu ya Vijana Stars inayotokea Ludewa
Mjini na kujinyakulia zawadi ya Mbuzi katika Ligi iliyokuwa kiendelea
wilayani Ludewa katika kata ya Ludewa Mjini.
Ushindi huo umekuja mara baada ya
mshambuliaji machachali wa timu hiyo Anton Malongo kuifungia timu
yake magili yote matatu na kutangazwa kuwa ndiyo timu iliyokuwa ina
point nyingi ikilinganishwa na timu nyingine zilizoshiriki katika
mashindano hayo.
Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na
kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Ludewa Edings Mwakambonja kwa
kushirikiana na Fransis Luoga na kuandaliwa na Hakimu wa wilaya ya
Ludewa Mh.Fredlick Lukuna yalizishirikisha timu 7 lengo likiwa ni
kukuza vipaji vya vijana katika mchezo huo wilayani Ludewa na
kupambana na Rushwa.
Timu zilizoshiriki ni pamoja na Nindi
fc nafasi ya mwisho,Mzalengo fcnafasi ya sita,Black stars nafasi ya
tano na Ludewa Rangers nafasi ya nnenyingine ni Vijana stars nafasi
ya tatu,Veterani nafasi ya pili na Town Stars ambayo ndiyo mshindi wa
mashindano hayo.
Aidha mgeni rasmi katika fainali ya
ligi hiyo ambaye ni OCD wa wilaya ya Ludewa Emmanuel Galiyamoshi
alisema mashindano hayo yameonesha jinsi gani vijana wanavipaji kwani
kila timu ilikuwa ikibadirika kila siku na kuwa bora hivyo wadau
mbalimbali wanatakiwa kujitolea kuanzisha mashindano kila wakati.
Kamanda Galiyamoshi alisema licha ya
kuwa kulikuwa na ushindani lakini vijana walipata mahali pa kupotezea
muda na kuachana na uharifu ambao ungeweza kujitokeza mitaani na
kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Naye Kamanda wa TAKUKURU Edings
Mwakambonja alisisitiza kuwa katika mashindano hayo vijana wanatakiwa
kujua rushwa ni adui wa haki na haikubariki nchini hivyo kila kijana
anatakiwa kuwa mlinzi mwa mwenzie katika hilo.
Alisema kama vijana wataungana kupinga
Rushwa kwa sauti moja basi hakuna mtu ambaye atapenya na kufanya
vitendo vya rushwa kwani anaweza kushughurikiwa na vijana wenyewe kwa
kutoa taarifa katika ofisi yake haraka.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment