Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 28, 2017

PROF.LUDWIG KUTOKA UJERUMAN AITEMBELEA SHULE YA MRNING STAR WILAYANI LUDEWA.

 Prof.Ludwig akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Morning star
 Karibu Shule ya Morning Stara


  Prof.Ludwig akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Morning star

Mkurugenzi wa shirika la PADECO Bw.Wilbad Mwinuka akisalimiana na walimu wa Morning star





Shule ya Mrning star iliyoko wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ambayo ni shule ya awali na Msingi inayomilikiwa na mtu binafsi imepata Fulsa ya kutembelewa na Prof.Ludwig kutoka nchini Ujeruman kutokana na shule hiyo kufanya vizuri katika masomo pia kuhudumia watoto wanaotoka katika mazingira magumu.

Akizungumza na baadhi ya wajumbe wa bodi,walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo Prof.Ludwig alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi nya shuleni hapo kwani amekuwa akifika wilayani Ludewa lakini hakuwahi kuitembelea shule hiyo ya watoto.

Alisema kuwa uwepo wa shule za watoto wadogo ni muhimu zaidi katika ustawi wa elimu kwani huko ndiko elimu inakoanza kupikwa hivyo ni muhimu wazazi wakajenga utamaduni wa kuwapeleka watoto wao wadogo katika shule za namna hiyo ili kuanza kujifunza Lugha mbalimbali.

Aidha Prof.Ludwig alisisitiza ujenzi wa mabweni kwani yaliyopo yahakidhi haja ya wanafunzi kwani kuna kila sababu ya kujenga mabweni ili shule hiyo isiruhusu wanafunzi wa kutwa na badala yake wote waishi bwenini.

Akisoma Taarifa ya shule  mratibu wa shule hiyo Bw.Augustino Mwinuka alisema kuwa richa ya kuwa shule hiyo ina madhari mazuri ya kujisomea lakini inachangamoto nyingi iliwemo ya ukosefu wa uzio ambao ni usalama zaidi kwa watoto.

Bw.Mwinuka alisema kuwa shule hiyo ni shule pekee binafsi ambayo inatoa elimu ya msingi katika kata ya Ludewa hivyo ni muhimu ikaungwa mkono na wadau mbalimbali wa elimu ili iweze kusonga mbele.

Hivyo alimuomba Prof.Ludwig kuweza kuiombea misaada kwa wadau mbalimbali nchini ujerumani ili kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo kwani unaeneo kubwa hivyo inaweza siku moja ikaongeza na madarasa ya Sekondari ili wanafunzi wanaopata elimu Morning star kuweza kupata na elimu ya sekondari hapo hapo.

Mwisho.

No comments: