Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 30, 2014

TIMU YA TOWN STARS YAIBUKA KIDEDEA KATIKA KOMBE LA MBUZI

 Hawa ndio Mbuzi wa zawadi ya mshingi wa kwanza na wapili
OCD Galiyamoshi ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mashindano hayo akiongea na wachezaji na mashabiki kabla ya kukabidhi zawadi ya mbunzi kwa washindi

Mmoja wa wasimamizi wa mashindano Bw.Jerome Bange akisoma taarifa ya mashindano kwa mgeni rasmi

 Kamanda wa TAKUKURU Edings Mwakambonja akiongea na wachezaji pamoja na mashabiki wa pambano hilo

Muandaaji wa mashindano hayo kulia Mh.Lukuna akiwa na wageni waalikwa pamoja na wadhamini wa mashindano hayo


vijana wa timu ya Town stars wakiwa na furaha baada ya kushinda
Waamuzi wakimsikiliza mgeni rasmi
Mgeni Rasmi akimkabidhi Mbuzi kongozi wa timu ya Town stars

Wachezaji wa timu ya Town stars wakifurahi kwa kumnyanyua Mbuzi juu baada ya kukabidhiwa
Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Edings Mwakambonja akiwa na washindi wa mashindano hayo yimu ya Town Stars katika picha ya pamoja

TIMU ya mpira wa miguu yenye makao yake makuu Ludewa mjini ijulikanayo kama Town Stars imeibuka kidedea baada ya kuichapa magli 3 kwa bila timu ya Vijana Stars inayotokea Ludewa Mjini na kujinyakulia zawadi ya Mbuzi katika Ligi iliyokuwa kiendelea wilayani Ludewa katika kata ya Ludewa Mjini.

Ushindi huo umekuja mara baada ya mshambuliaji machachali wa timu hiyo Anton Malongo kuifungia timu yake magili yote matatu na kutangazwa kuwa ndiyo timu iliyokuwa ina point nyingi ikilinganishwa na timu nyingine zilizoshiriki katika mashindano hayo.

Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Ludewa Edings Mwakambonja kwa kushirikiana na Fransis Luoga na kuandaliwa na Hakimu wa wilaya ya Ludewa Mh.Fredlick Lukuna yalizishirikisha timu 7 lengo likiwa ni kukuza vipaji vya vijana katika mchezo huo wilayani Ludewa na kupambana na Rushwa.

Timu zilizoshiriki ni pamoja na Nindi fc nafasi ya mwisho,Mzalengo fcnafasi ya sita,Black stars nafasi ya tano na Ludewa Rangers nafasi ya nnenyingine ni Vijana stars nafasi ya tatu,Veterani nafasi ya pili na Town Stars ambayo ndiyo mshindi wa mashindano hayo.

Aidha mgeni rasmi katika fainali ya ligi hiyo ambaye ni OCD wa wilaya ya Ludewa Emmanuel Galiyamoshi alisema mashindano hayo yameonesha jinsi gani vijana wanavipaji kwani kila timu ilikuwa ikibadirika kila siku na kuwa bora hivyo wadau mbalimbali wanatakiwa kujitolea kuanzisha mashindano kila wakati.

Kamanda Galiyamoshi alisema licha ya kuwa kulikuwa na ushindani lakini vijana walipata mahali pa kupotezea muda na kuachana na uharifu ambao ungeweza kujitokeza mitaani na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Naye Kamanda wa TAKUKURU Edings Mwakambonja alisisitiza kuwa katika mashindano hayo vijana wanatakiwa kujua rushwa ni adui wa haki na haikubariki nchini hivyo kila kijana anatakiwa kuwa mlinzi mwa mwenzie katika hilo.

Alisema kama vijana wataungana kupinga Rushwa kwa sauti moja basi hakuna mtu ambaye atapenya na kufanya vitendo vya rushwa kwani anaweza kushughurikiwa na vijana wenyewe kwa kutoa taarifa katika ofisi yake haraka.

Mwisho.

No comments: