Mh.Edward Haule akifanya harambeeya fedha kwaajili ya kutatua kero ya maji shuleni hapo
viongozi mbalimbali wakifuatilia maonesho katika sherehe hizo
Mh.Edward Haule akiwa na Makamu mkuu wa shule wakifafanua jambo
diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo akimshukuru mgeni rasmi
hawa nia baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita
Wahitimu wa kidato cha sita wakiimba nyimbo za kwaya
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi,viongozi wengine pamoja na wahitimu
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi,viongozi wengine pamoja na wahitimu
Ukosefu
wa maji safi na salama katika shule ya sekondari Chief Kidulile iliyoko katika wilaya ya Ludewa
Mkoani Njombe umetajwa kuwa ni changamoto kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo
hali inayosababisha wakati mwingine kulazimika kuvunja vipindi ili wanafunzi kwenda
kuchota maji mtoni.
Hayo
yamesemwa leo katika mahafari ya pili ya kidato cha sita na makamu mkuu wa
shule hiyo mwalimu Benitho Mahenge wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi ambapo
alizitaja changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo ambazo ni ukosefu wa
Dahalia,nyumba za walimu,bwalo la chakula na ukosefu wa maji safi na salama.
Mwalimu
Mahenge alisema kuwa shule iyo ambayo iko katika makao makuu ya wilaya imekuwa ni miongoni mwa shule bora wilayani
Ludewa ,lakini tatizo la maji safi na salama limekuwa kubwa kwani kuna wakati
inawalazimu kuwatoa wanafunzi madarasani ili kutafuta maji ya kuandalia chakula
hali ambayo ni kero kubwa kwa wanafunzi hao.
Alisema
kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji safi na salama linapelekea baadhi ya
wanafunzi kuugua homa za matumbo hivyo alimuomba mgeni rasmi kuliangalia jambo
hilo ambalo ni kero kubwa lakini pia bwalo la chakula kwani msimu wa mvua huwa
shida kwa wanafunzi hivyo hulazimika kutumia madarasa kama bwalo la chakula.
Akitoa
Hotuba yake katika mahafari hayo mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri
ya wilaya ya Ludewa Mh.Edward Haule alisema kuwa chule hiyo ni kioo cha wilaya
ya Ludewa kutokana na ukweli kwamba ipo makao makuu ya wilaya hivyo ni aibu
kuonekana haina maji safi na salama.
Mh.Haule
alisema kuwa tayari amewasiliana na Mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa na kupewa
makisio ya utatuzi wa tatizo la maji chief kidulile ambayo gharama yake haizidi
shilingi milioni mbili na Nusu,hivyo alitoa kiasi cha shilingi laki mbili na
kuwaomba wageni waliohudhuria mahafari hayo kumuunga mkono ambapo jumla ya
shilingi 564000/=zilipatika kama halambee.
Mh.Haule
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni diwani wa kata ya
Ibumi aliwaomba wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo pamoja na wakazi
wa mji wa Ludewa kuichangia shule hiyo ili kumaliza tatizo ambalo ni kero kubwa
kwani tayari kiasi kidogo kimeshachangwa katika sherehe hizo za mahafari.
“Naomba
wazazi tuungane kutatua kero hii ambayo tunauwezo nayo kwa kuchangishana ili
kuwanusuru watoto wetu na homa za matumbo,lakini kwa yale makubwa Diwani wa
kata kwa kushirikiana na Mbunge Mh.Deo Ngalawa wanachapa kazi kwa kutafuta
wafadhiri mbalimbali ili kuzimaliza kero hizo pia mimi kama mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya na Serikali ya wilaya ya Ludewa tutahakikisha kero hizo
zinatatuliwa”,alisema Mh.Haule.
Alisema
kuwa tayari kuna mfadhiri amejitokeza kujenga mabweni mawili lakini wananchi
wanatakiwa kuandaa mchanga,Tofari na mawe hivyo kinachotakiwa ni kujitoa kwa
moyo katika kazi hizo ili kuwafanya wanafunzi wote kuishi bwenini pia aliwataka
wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kwenda kujitolea katika shule walizotoka
ili kuwasaidia wadogo zao.
Mwisho.
KWA UDHAMINI WA MTANZANIA RESTAURANT, WANAPATIKANA LUDEWA MJINI KATIKA JENGO LA NDICHELIWE.
KWA CHAKULA SAFI NA BORA UKIFIKA LUDEWA MJINI MTANZANIA RESTAURANT NDIO SURUHISHO PIA KWA CHAKULA CHA MAHARUSI,MISIBA MAHAFARI NA SHEREHE MBALIMBALI
KWA MAWASILIANO PIGA NO.0758146258 au 0624985168 KWA CHAKULA CHA UHAKIKA.
No comments:
Post a Comment