Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dakt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa chuo cha Veta wilayani Makete
Wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete
Hili ni moja ya jengo la Veta wilayani Makete
Rais kikwete akiweka jiwe la msingi katika chuo cha VETA wilayani Makete
Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana alizindua chuo cha VETA
ikiwa ni chuo cha kwanza katika mpango wa Serikali wa kuhakikisha kila wilaya
inakuwa na chuo cha ufundi staid ili kuhakikisha vijana wanapata fulsa ya ujuzi
mbalimbali.
Akisoma taarifa ya
ujenzi wa chuo hicho mkurugenzi mkuu wa VETA Tanzania Bw.Moshi katika ziara ya
Rais katika wilaya za mkoa wa Njombe alisema chuo hicho kimejengwa kwa
ushirikiano wa Halmashauri ya wilaya ya Makete na VETA taifa.
Alizitaja gharama za
ujenzi wa chuo hicho hadi kukamilika ni shilingi 2.29 bilion ambapo alibainisha
kuwa fedha taslimu ni shilingi 1.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi na shilingi 785
milioni zilitumika kama gharama za vifaa.
Bw.Moshi alisema mchango
wa Halmashauri ya wilaya ya Makete ni pamoja na utengenezaji wa barabara
ya kufika chuoni hapo,maji kwaajili ya ujenzi,umeme, mawe na mchanga pamoja na
nyumba ya kuishi mafundi.
Alisema chuo hicho
kimejengwa na wanafunzi pamoja na walimu wao kutoka chuo cha VETA Mpanda ambao
wamefanya kazi kubwa wakishirikiana na wananchi katika kuhakikisha ujenzi
huo unakamilika mapema kwa muda uliopangwa.
“chuo hiki ni cha kwanza
katika mpango wa Serikali wa kujenga vyuo vya VETA katika kila wilaya kati ya
vyuo vingi kikiwemo chuo cha VETA wilayani Ludewa na kile cha Mkoa ambacho
kitajengwa katika mji wa Njombe hivyo ni fulsa pakee kwa wananchi kupata kozi
mbalimbali”,alisema Bw.Moshi.
Alizitaja changamoto
zinazoikumba taasisi ya VETA ni pamoja na sheria ya manunuzi inayowataka
kununua mitambo na vifaa vipya vya kujifunzia ambapo uwezo wa VETA kununua
vifaa hivyo ni mdogo ukilinganisha na bajeti wanayoipata.
Bw.Moshi alisema katika
somo la ufundi wa mitambo,magari na dege wanalazimika kununua injini mpya ili
kuwawezesha wanafunzi kujifunzia hivyo alimuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania kuliomba Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania kulegeza
masharti hayo yatakayowawezesha kutoa elimu kwa ufanisi zaidi.
Katika hotuba yake Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dakt Jakaya Mrisho Kikwete alilipokea
ombi hilo na kuahidi kulifanyia kazi kutokana na uzito wa jambo hilo linalorudisha
nyuma juhudi za ufundishaji kwasababu ya masharti ya sheria ya manunuzi.
Dkt.Kikwete alisema
mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila wilaya inakuwa na chuo cha VETA ili
kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata fulsa ya kujiajili na kuajiliwa
kwani elimu ndio msingi wa maisha ya mtanzania.
Katika ziara hiyo Dkt
Kikwete licha ya kuzindua chuo cha VETA pia aliweza kuzindua zahanati,shule ya
Sekondari Lupalilo yenye kidato cha tano na sita ambayo ilijengwa mwaka 1911 na
kanisa la KKKT na kuwa shule ya kwanza wilayani Makete.
Dkt Kikwete aliwataka
wananchi wilayani humo kuzitumia fulsa za elimu hasa katika kujiunga na masomo
chuoni hapo ili kuweza kupata ujuzi wa kutengeneza vitu mbalimbali
vinavyotokana na mazao ya miti na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.
Alisema wilaya ya Makete
inaongoza kwa kilimo cha viazi hivyo ni jambo la msingi kama chuo hicho
kitafundisha kozi zinazoendana na mazingira halisi ya mazao ya maeneo hayo
baada ya kusafirisha viazi vibichi kwa kuvipeleka Dar es Salaam.
“Kwa ujenzi huu wa chuo
cha VETA wilayani hapa ni ukombozi mkubwa kwa vijana wenu kwani wataweza
kujifunza ufundi mbalimbali hasa katika kutengeneza samani kwa ni moja ya
wilaya nchini inayozalisha mbao pia utengenezaji wa chipsi na kuziweka katika
vifungashio na kuziuza nchini na nje ya nchi”,alisema Dkt Kikwete.
No comments:
Post a Comment