Hii ni ngoma mpya anayotarajia kuiachia hivi karibuni itakayotambulika kwa jina la Kidonda changu
Huyu ndiye Addy Ng'ari msanii maarufu wa bongo fleva mkoani Njombe
Msanii
maarufu mkoani Njombe wa muziki wa Bongo Fleva anayejulikana kwa jina la Addy
Ng’ari amerudi kivingine,baada ya ukimya wa muda mrefu katika muziki kutokana
na kubwana na mambo yakifamilia.
Addy Ng’ari
aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali zikiwemo Ua,Nyumba yakupanga,Tanzania nchi
yangu,Maisha na ile ya Ni kweli napenda lakini hasa kibao cha Niamini ambacho
mpaka leo kibao hicho bado kinatamba katika maeneo mbalimbali nchini na nyimbo
hizo zinapatikana katika mtandao wa you tube.
Akiongea na
waandishi wa habari Msanii Addy Ng’ari alisema kuwa kumekuwa na uvumi kuwa
ameachana na saana baada ya kufiwa na mpendwa wake aliyemdhamini kufanya kazi
mbalimbali katika studio kubwa nchini marehemu Deo Filikunjombe lakini yeye
bado anafanya sanaa na hivi ameamua kurudi kivingine na kutoa ngoma mbili
mfululizo.
Alisema kuwa
ni kweli amepata pigo kubwa kuondokewa na Flikunjombe ambaye ndiye alikuwa
akimuunganisha na studio mbalimbali na ilimbidi kusimama kwa muda katika
sanaa,hivyo amewataka mashabiki wake kutokuwa wanyonge kwani mchango wake
kisanaa katika mkoa wa Njombe ni mkubwa kutokana na wasanii wengi wachanga
kufuata miondoko yake.
“Ni kweli
nimepata pigo kwa kufiwa na mtu aliyekuwa ni msaada kwangu Mh.Filikunjombe na
baada ya kupata taarifa za msiba wake ilinibidi kutunga nyimbo ya maombolezo
ambayo ndio ilipigwa katika vyombo mbalimbali vya habari na pale msibani na
ikanilazimu kusimamisha kazi zangu za sanaa kwa muda,lakini niwaeleze mashabiki
wangu nimerudi kivingine wategemee burudani kama kawaida,”alisema Addy Ng’ari.
Addy Ng’ari
alisema kuwa tayari ameshatoa kibao kipya ambacho kinatamba mtaani ambacho
kinakwenda kwa jina la Umri unasonga na kibao kingine kipo njiani ambacho sio
muda mrefu atakiachia kitakachotambulika kwa jina la Kidonda Changu.
Aidha amewataka
wasanii wote nchini kudumisha umoja na mshikamani ili kukuza sanaa mkoani hapa kwani
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali anatarajia kufanya matamasha makubwa katika
mikoa mnne ambayo yanalengo la kuibua vipaji vipya atashirikisha wasanii mbalimbali nchini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment