Bw.Nickson Mahundi akikabidhi misaada mbalimbali kwa walimu ya shule maalumu ya Mundindi
Bw.Nickson Mahundi akikabidhi msaada wa nguo kwa Diwani wa viti maalumu tarafa ya Liganga kwajili ya wanafunzi wa shule maalumu ya Mundindi
Wafanyakazi
90.3 best fm radio Ludewa kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali waishio Ludewa mjini wamesherehekea sikukuu ya
Pasaka na wanafunzi wa shule maalumu ya Mundindi iliyoko kata ya Mundindi
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kwa kutoa vitu mbalimbali kwa wanafunzi
hao.
Akikabidhi
vifaa hivyo zikiwemo Daftari,Dawa za Maswaki,mafuta ya Kupakaa,Sabini na Nguo
meneja wa kituo cha radio best fm na Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa Mkoa
wa Njombe Bw.Nickson Mahundi alisema kuwa kutokana na mahitaji ya wanafunzi wa
shule hiyo uongozi wa radio best fm uliona umuhimu wa kuwashirikisha wadau
mbalimbali katika kuwasaidia watoto hao.
Bw.Mahundi
alisema kuwa shule hiyo pekee Maalumu ya wilaya ya Ludewa ni shule inayotakiwa
kuonwa kwa jicho la pekee kutokana na mahitaji halisi ya wanafunzi wanaosoma
katika shule hiyo kwani bado jamii haitambui elimu gani inayotolewa katika
wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Alisema kuwa
bado jamii haina mwamko wa kuwatembelea wanafunzi hao na kuwajulia hali
kutokana na shule hiyo kumilikiwa na Serikali lakini ukweli ni kwamba watoto
wanaosoma shule hiyo wanatoka vijiji mbalimbali ndani na nje ya wilaya pia
wanatoka katika familia masikini ambazo hazina uwezo hata wakuwatembelea hivyo
wadau mbalimbali wanatakiwa kujitolea katika kuwasaidia watoto hao kwa kuwa
Serikali inatoa baadhi tu yamahitaji.
“Tumekuja
kuwatembelea na kutoa vitu hivi vichache ambavyo ni michango ya wafanyakaji wa
wa radio best fm na viongozi wao lakini pia kuna michango ya wadau wa radio
yetu wanaoishi Ludewa mjini na vijijini lai yangu ni kwa jamii itambue kuwa
hawa wanafunzi ni wetu hivyo tunapaswa kuwasaidia kwani mtoto wa mwenzio ni
wako”,alisema Bw.Mahundi.
Naye mwalimu
wa shule hiyo Tumaini Mapunda akitoa taarifa ya shule alisema kuwa shule hiyo
ina kabiliwa na upungufu mkubwa wa mabweni kwani mabweni yaliyoko hayaendanina
idadi ya wanafunzi hali inayo walazimu kuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi
ambao nihatari kwa afya zao.
Mwalimu Mapunda
alisema kuwa shule hiyo ina wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbalimbali kama
vile wasioona,wasiosikia,wenye mtindio wa ubongo, wenye ulemavu wa ngozi na
wenye ulemavu wa viungo hivyo kuna walimu wenye mafunzo maalumu ambao wana
uwezo mkubwa waku wafundisha wanafunzi wao.
Alisema kuwa
wazazi wawanafunzi hao wamekuwa na maisha magumu hali inayo sababisha
halmashauri ya wilaya ya ludewa kutumia
baeti kubwa katika kuwarudisha makwao shule inapo fungwa na kwenda kuwachukua
shule inapo funguliwa aidha aliwashukuru wadau mbalimbali wanao jitolea katika
kuwasaidia wanafunzi hao.
Akiushukuru
uongozi wa radio Best fm Ludewa kwa kuwatembelea na kutoa misaada kwa wanafunzi
hao diwani wa kata ya Mundindi kupitia chama cha mapinduzi (CCM),Mh.Wise Mgina
alisema kuwa tokea shule hiyo ianzishwe hakuna waandishi wowote ambao wamewahi
kutembelea shuleni hapo.
Mh. Mgina
aliupongeza uongozi wa redio Best fm kwa ziara iyo na kuutaka uendelee
kuitangaza shule hiyo na changamoto zake katika maeneo mbalimbali ili wadau
waweze kujitokeza kutoa misaada na kuiga mfano wa radio Best fm kwani ni
wananchi pekee wa kata ya Mundindi ndio wanaowajibika katika ujenzi wa shule
hiyo richa ya kuwa kuna wanafunzi wa maeneo mbalimbali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment