Kikao cha KAMAKA kikiwa kinaendelea katika kijiji cha Nindi kwaajili ya kupata hati za kimila za Ardhi
Afisa ardhi mteule wa wilaya ya Ludewa Bw.Joseph Kamonga akikabidhiwa zawadi maalum kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Nindi Bw.Henjewele akiwa na Mkewe
Vijana wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata mafunzo ya kutumia GPS
WANANCHI wa kijiji cha
Nindi kata ya Lupingu wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe hivi
karibuni wanatarajia kunufaika na hati za kimila katika umiliki wa
Ardhi kutokana na wataalamu wa halmashauri ya Ludewa kuanza zoezi
hilo katika kijiji hicho.
Akizungumza katika kikao
cha kamati ya halmashauri ya kijiji(KAMAKA) kilichofanyika jana
kijijini hapo Mwenyekiti wa kijiji cha Nindi Bw.Valentin Henjewele
alisema hatua hiyo itaondoa migogoro iliyokithiri kijijini hapo kwa
muda mrefu.
Bw.Henjewele alisema
viongozi wa kijiji hicho wamekuwa wakipata usumbufu wa kutatua
migogoro hivyo hatua iliyofikiwa na Serikali ya kuandaa mpango wa
matumizi bora ya Ardhi katika kijiji chake itakuwa ni ukombozi mkubwa
hasa kwa raia ambao walikuwa hawajui sheria na mipaka yao.
Alisema upimaji huo wa
ardhi na umiliki wa hati za kimila utakuwa ni chachu ya maendeleo kwa
vijiji jirani ambavyo bado havijapimwa kwani wataalamu wa ardhi toka
wilayani wameweza kufafanua faida za hati hizo ambapo wajumbe wa
mkutano huo wamepata shauku ya kumiliki hati hizo.
“Tunaishukuru Serikali
kwa suala hili kwani wananchi kupitia hati hizi za kimila wataweza
kukopesheka na asasi mbalimbali za kifedha tofauti na miaka ya nyuma
tulikuwa tukigombania ardhi bila manufaa yoyote lakini kwa sasa hata
migogoro miongoni mwetu ya kuhusiana na mipaka itapungua”,alisema
Bw.Henjewele.
Afisa Ardhi Mteule wa
wilaya ya Ludewa Bw.Joseph Kamonga mpango wa utoaji wa hati za kimila
za umiliki wa ardhi kwa wananchi ni endelevu kwani mpaka sasa tayari
vijiji vitatu vimesha pimwa na tayari hati zinaandaliwa.
Bw.Kamonga alisema
Serikali imeona umuhimu wa kupima ardhi ya vijiji na kutoa hati kwa
wananchi ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima kwa wananchi kutokana
na thamani ya ardhi inavyoongezeka siku hadi siku.
Mradi huo unasimamiwa na
Halmshauri ya wilaya ya Ludewa baada ya kujengewa uwezo na MKURABITA
hivyo umeanza kwa vijiji vya mfano ambavyo ambavyo ni Iwela,Aman na
Nindi ili kuiwezesha zamii kunufaika na ardhi.
Alisema hati hizo za
kimila zitawapa fulsa mbalimbali wananchi kutokana na umuhimu wa hati
hizo hivyo mtu yeyote mwenye hati hiyo atakuwa na uwezo wa kukopa
fedha bank na kuiwekea dhamana hati hiyo.
Bw.Kamonga alisema licha
ya wananchi wa kijiji cha Nindi kunufaika na hati hizo lakini kupitia
upimaji wananchi hao wataweza kujifunza sheria za ardhi kutokana na
ushiriki wao katika upimaji pia watajua mipaka ya kijiji chao na
vijiji vingine kwa ufasaha.
Alisema baadhi ya wananchi
wamepata mafunzo ya kutumia vifaa vya upimaji kama gps ambao
watashiriki moja kwa moja na wataalamu watakaohusika na zoezi hilo la
kupima kuanzia wiki la jumatatu ambapo baada ya kumaliza wananchi
wataweza kuandaliwa hati zao na kukabidhiwa.
Aidha aliwataka wananchi
hao kuzitunza hati watakazo pata kwani zisipotunzwa inaweza kuibuka
migogoro mingine baadae na ushahidi ukakosekana kwa lengo la kutafuta
suruhu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment