Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 10, 2015

VIJANA WILAYANI LUDEWA WASHINDWA KUTUMIA FULSA YA ELIMU

hii ndio shule ya Sekondari Masimbwe aiko wilayani Ludewa kata mpya ya Lubonde
 Mkuu wa shule ya Masimbwe Mwalimu Eliud Sanga

Cheti ambacho ni daraja C ambacho kimetolewa na VETA kwaajiri ya kuruhusu elimu ya ufundi itolewe katika shule hiyo

 darasa la ufundi ushonaji


darasa la ufundi magari
 darasa la masomo ya kawaida ya sekondari

 darasa la komputor
mwalimu  mkuu wa shule ya masimbwe Eliud Sanga











Imeelezwa kuwa vijana wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameshindwa kutumia fulsa ya kielimu kwa kile kinachodaiwa kuwa  wilaya ya Ludewa kuwa na shule ya Sekondari inayotoa elimu ya sekondari na ufundi mbalimbali lakini vijana wengi wa wilaya hii kushindwa kuitumia shule hii ipasavyo na kuendelea kulalamika kuwa wilaya ya Ludewa bado haina chuo cha ufundi.


Shule hiyo ambayo inamilikiwa na umoja wa wazazi nchini wa chama cha mapinduzi inatoa elimu ya sekondari na mafunzo ya ufundi kwa wakati mmoja ijulikanayo kwa jina la Masimbwe Sekondari imekuwa ikipata ufadhiri mkubwa kutoka kwa raia wa nchi ya Ujerumani Prof.Ludwige amekuwa akileta zana mbalimbali za kufundishia masomo ya ufundi karibu kila na kuwalipia ada wanafunzi waishio katika mazingira magumu imekuwa na wanafunzi wachache tofauti na matarajio ya uanzishwaji wa shule hiyo.


Akiongea na waandishi wa habari mapema wiki hii mkuu wa shule hiyo Mwalimu Eliud Sanga alisema kuwa shule hiyo ni shule pekee katika mkoa wa Njombe ambayo mwanafunzi anahitimu kidato cha nne na kutoka na vyeti viwili ambavyo ni cheti cha kidato cha nne na kile cha veta ambapo mwanafunzi anayehitimu kitado cha nne katika shule hiyo anauwezo wa kuomba ajira katika ofisi mbalimbali.


Mwalimu Sanga alisema kuwa vijana walio wengi wilayani hapa  wamekuwa mabingwa wa kulalamika na kusema wilaya ya Ludewa haina chuo cha ufundi hali ambayo sio sahihi kwani shule hiyo licha ya kutoa elimu ya sekondari pia inatoa mafunzo ya ufundi tu ya muda mfupi wa miezi mitatu mitatu lakini cha kushangaza wanaosoma shule hiyo ni wanafunzi wa mikoa ya mbali ndio wanaojua kutumia fulsa.


Alisema mpaka sasa kuna baadhi ya vifaa vulivyoletwa na mfadhiri Prof.Ludwige havijafunguliwa katika makontena kutokana na uhaba wa wanafunzi pia kuna baadhi ya wanafunzi waliosoma katika shule hiyo ya Masimbwe tayari wameshaajiriwa  katika ofisi mbalimbali baada ya kuhitimu kidato cha nne ikiwemo ofisi ya shirika la Tanesco Ludewa mjini pia mradi wa umeme LUMAMA kata ya mawengi.


“inashangaza kuona vijana wa Ludewa pamoja na wazazi kushindwa kutumia fulsa hii ambayo iko jirani na badala yake wananufaika vijana wa mikoa ya mbali kwani mfadhiri wa shule hii analeta vifaa vya ufundi magari,umeme,ushoonaji, ujenzi na komputor akiwa na lengo la kuwainua vijana wa wilaya ya Ludewa ili baadae waweze kuajiliwa katika migodi ya chuma na makaa ya mawe lakini juhudi zake zinaonesha kukatishwa tamaa na wanaludewa wenyewe”,alisema Mwalimu Sanga.


Mwalimu Sanga alisema kuwa mpaka sasa mfadhiri wa shule hiyo Prof.Ludwige anawalipia ada wanafunzi wapatao 25 kila mwaka ambao wanatoka katika mazingira magumu wengi wao wakitokea mikoa ya mbali kutokana na vijana wa wilaya ya Ludewa kutojitokeza kujiunga na masomo katika shule hiyo.


Alisema kuwa hata baadhi ya viongozi wa Serikali wilayani hapa hawajui kinachoendelea katika shule ya Sekondari Masimbwe hivyo aliwataka viongozi hao kuitembelea shule hiyo na kuona masomo yanayotolewa kwani inawalimu wa kutosha pia inafaulisha vizuri na kuhusu idikadi ya kisiasa mwalimu Sanga alisema kuwa elimu haina siasa hivyo shule hiyo haibagui wanafunzi wanaosoma hapo wametoka kadika familia zenye itikadi ya chama gani.


Mwisho.

No comments: