Wananchi wa kijiji cha Nkwimbili pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Edward Haule wakichimba barabara ya kuunganisha na makao makuu ya wilaya.
Wananchi wa kijiji cha Nkwimbili pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Edward Haule wakichimba barabara ya kuunganisha na makao makuu ya wilaya.
Wananchi wa kijiji cha Nkwimbili pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Edward Haule wakichimba barabara ya kuunganisha na makao makuu ya wilaya.
Mhariri wa Radio Best radio Ludewa Albentino Kayombo akiwa katika kijiji cha Nkwimbili
Mwandishi wa mtandao huu Nickson Mahundi akiwa katika kijiji cha Nkwimbili
Ukosefu wa
miundombinu ya barabara katika kijiji cha Nkwimbili kata ya Lupingu wilayani
Ludewa mkoa wa Njombe umewafanya wananchi wa kijiji hicho pamoja na viongozi wao
kuanza kufikilia mbinu mbadala ili huduma hiyo iweze kuwakomboa baada ya muda
mrefu kubeba wagonjwa wao katika machela.
Akiongea na
waandishi wa habari jana waliokitembelea kijiji hicho na kushiriki uchimbaji wa
barabara kwa jembe la mkono mwenyekiti wa kijiji cha Nkwimbili Bw.Augustino
Mlazo alisema kuwa tokea uhuru wa Tanganyika takribani miaka 57 imepita kijiji
hicho hakikuwahi kuwa na miundombinu ya barabara.
Bw.Mlazo
alisema kuwa wananchi wa kijiji hicho wamekuwa na shauku kubwa ya kuwa na
barabra ili kuviwezesha vyombo vya usafiri vikiwemo pikipiki na magari kuingia
kijijini hapo hivyo kwa umoja wao wameamua kushirikiana kwa kuanza kuchimba
barabara kwa jembe la mkono ili kuweza kuunganishwa na makao makuu ya wilaya ya
Ludewa.
Alisema kuwa
kijiji hicho chenye changamoto nyingi lakini wananchi kwa pamoja wameona
changamoto kubwa ni miundombinu ya barabara
ambayo kukosekana kwa barabara kumewafanya muda mwingi kutembea kwa
umbali wa Zaidi ya kilometa 20 kufuata huduma za kijamii.
“tangia nchi
hii ipate uhuru mwaka 1961 mpaka leo hatujawahi kuwa na barabara hivyo kutokana
na mazingira ambayo tunaishi tumeamua kufanya maendeleo ya kuchimba barabara
ili kupata huduma ya usafiri tunamshukuru mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
ya Ludewa kwa kutuunga mkono maana tunashiriki naye katika kazi hii tukitumia
jembe la mkono”,alisema Bw.Mlazo.
Aidha
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Diwani wa kata ya
Ibumi Mh.Edward Haule aliwasifu wananchi hao kwa umoja wao bila kulazimishwa na
mtu yeyote kwa kujitolea kuchimba barabara hiyo ambayo itawasaidia katika mambo
mbalimbali.
Mh.Haule
alikili kuwa kijiji hicho tangia Dunia iumbwe hakikuwahi kuwa miundombinu ya
barabara hivyo kutokana na umoja wao na kuona barabara ni hitaji la msingi
wameanza kuchimba kwa mkono ili kuunganisha na makao makuu ya wilaya ingawa
kunachangamoto nyingi ikiwemo ya milima mikali na maporomoko.
Alisema kuwa
kutokana na juhudi hizo za wananchi tayari Serikali imewaunga mkono kupitia
mradi wa Tasaf kwa kuombea fedha za upanuzi wa barabara hiyo kwani mpaka sasa
mashine ya kufanya upanuzi imeshaanza kazi kuanzia Ludewa mjini na imeshafikia
katika kitongoji cha Liwili karibu na kijiji hicho cha Nkwimbili.
Mh.Haule
aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo hasa wazaliwa wa kijiji hicho waishio
maeneo mbalimbani ndani ya nchi na nje kuunga mkono duhudi hizo za wananchi
kwani uwepo wa barabara hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kijiji cha
Nkwimbili kutokana na kadhia wanayoipata ya kubeba wagonjwa kwenye machela pale
hali inapokuwa mbaya.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment