Mwenyekiti
wa umoja wa wazazi wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Bw.John Kiowi
amewata wananchi wilayani hapa kuchangamkia fulsa ya kilimo cha Parachichi
kutokana na zao hilo kuwa zao la kibiasha na limeanza kuonesha matumaini katika
soko la ndani ya nchi na nje.
Hayo alisema
jana siku ya jumuhia ya wazazi nchini ambapo kama wilaya ya Ludewa maazimisho
hayo yamefanyia kata ya Ludewa mjini katika shamba la jumuiya hiyo lililopo
maeneo ya shule ya Sekondari Ludewa ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo pamona
na wananchi walijitokeza kulisafisha shamba lao.
Bw.Kiowi alisema
kuwa maadhimisho hayo yalipaswa yafanyike tarehe 6 April mwaka 2018 kutokana na
jumuiya hiyo ilianzishwa tarehe 6 April 1955 hivyo kutokana na kuwepo majukumu
mengi imelazimu kuazimisha leo tarehe jana kwa kufanya usafi katika shamba la
Parachihi.
Alisema kuwa
wananchi wa wilaya ya Ludewa bado haijatambua umuhimu wa kilimo za zao hilo
tofauti na wilaya nyingine za mkoa wa Njombe kama wilaya ya Wanging’ombe na
Njombe Dc ambazo wananchi wake wameanza kunufaika na zao la Parachicchi kwa
kujikwamua kutoka katika wimbi la umasikini.
“wilaya ya
Ludewa ni kati ya wilaya nchini zenye udongo wenye rutuba nzuri ambao unakubali
kilimo za mazao ya aina mbalimbali ukiangalia upende wa milimani ambako
kunabaridi kali ni vyema wananchi wake wakajikita katika kilimo cha parachichi
lakini kwa upande wa bondeni mwambao wa ziwa Nyasa kilimo cha Korosho
kinakubali hivyo nao wanapaswa kuchangamkia fulsa hiyo”,alisema Bw.Kiowi.
Naye katibu
wa umoja wa wazazi wilaya ya Ludewa Bi.Veronika Bilia alisema kuwa umoja huo kwa
wilaya ya Ludewa umekuwa na miradi mingi zikiwemo shule za Sekondari pamoja na
mabwawa ya samaki hivyo ni vyema wazazi wakajua umoja huo ni funzo kwa wazazi
walio wengi kutokana na hali halisi ya umuhimu wa mzazi katika familia.
Bi.Veronika
alisema kuwa mwananchi yeyote mwenye umri wa kuanzia mika 18 na kuendelea
anatakiwa kujiunga na jumuiya ya wazazi bila kubagua jinsi hivyo ofisi ya
jumuiya ya wazazi wilaya ya Ludewa inamipango mingi katika miradi endelevu
ikiwemo upandaji wa miti ya mbao kwa manufaa ya vizazi vijavyo kama katibu
ofisi ipo wazi kwa anayetaka kujiunga na jumuiya hiyo anakaribishwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment