Meneja wa mamlaka ya maji Ludewa Bw.Mwinuka Gregory akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Pets
wajumbe wa pets wakiongea na mkandarasi
Hili ndilo eneo linalojengwa tank la maji
Hili ndilo eneo linalojengwa tank la maji
hiki ndicho chanzo cha maji
Wajumbe wa
PETS katika kata ya Ludewa Mkoani Njombe wameanza kazi ya kuitembelea na
kuikagua miradi ya mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ukiwemo
mradi mkubwa wa maji utakao wanufaisha
wananchi wa kijiji cha Ludewa mjini.
Akiongea na
wanahabari jana katibu wa kamati ya pets Ludewa Bw.Alen Msigwa alisema kuwa
PETS ni kamati maalumu inayoundwa na viongozi kutoka Dini na Madhehebu
mbalimbali ili kusimamia na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo
inayotekelezwa eneo husika na kutolea taarifa kwa wananchi katika mikutano ya
vijiji.
Bw.Msigwa
alisema kuwa kumekuwa na maswali mengi baina ya wananchi wa kijiji cha Ludewa
kuhusiana na mradi mkubwa wa Maji ambao ni muhimu kwa wakazi wa Ludewa kutokana
na kutokuwa na taarifa sahihi umeanza linin a unatakiwa kukabidhiwa lini kwa
wananchi,hivyo kupitia pets wananchi watapata majibu sahihi kutoka kwa
wataalamu.
Alisema
mradio huo ambao unaghalimu Zaidi ya shilingi milioni mia nne umekuwa
ukizungumziwa sana na wananchi kutokana na shauku kubwa ya wananchi hao
kujikwamua na tatizo la maji ambalo lilikuwa ni kilio cha wananchi kwa muda
mrefu.
“tumetembelea
na katika ukaguzi wetu tumeweza kuona maendeleo mazuri katika ujenzi wa mradi
huu richa ya kuwa kumekuwa na maneno ya hapa na pale kuwa mkandarasi
anacherewesha ujenzi na ndio sababu iliyotufanya sisi kuja kukagua,ukweli ni
kwamba mkandarasi yuko vizuri na tunatumaini ataumaliza mradi huu mapema Zaidi”,alisema
Bw.Msigwa.
Akitolea
taarifa ya mradi huo meneja wa mamlaka ya maji mji wa Ludewa Bw.Gregory Mwinuka
alisema kuwa mradi huo wa maji ujulikanao kwa jina la Mdonga unajengwa na
kampuni ya Cviliano co.Ltd ya jijini Mwanza ambayo kiuhalisia inaoneka iko
vizuri kutokana na maradi huo kujengwa haraka.
Alisema
mpaka sasa tayari bomba zimeshatandikwa na zoezi linaloendelea kwa sasa ni ujenzi
wa tank kubwa ambalo litasambaza maji katika vitongozi vya Kiyombo,kanisa
B,Kanisa A na kitongojo cha Kimbila kwani wananchi wa vitongoji hivi wamekuwa na
uhitaji mkubwa wa huduma ya maji safi na salama baada ya kuikosa kwa muda.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Civiliano Co.Ltd Mhandisi Seleman Waziri akielezea
changamoto anazokumbana nazo katika mradi huo alisema kuwa kumekuwa na
changamoto katika upatikanaji wa vifaa kutokana na ukweli kwamba wanunuzi wa
vifaa ni Iruwasa hivyo vifaa huchelewa kuletwa hali inayomfanya kuchelewesha
kazi.
Aidha
aliwasifu wananchi wa wilaya ya Ludewa kwa ushirikiano anaoupata kwani maeneo
mengine kumekuwa na ugumu wa kazi lakini tofauti na wananchi wa Ludewa ambao
mara nyingi wamekuwa wakimfuata na kumshauri pale wanapoona kunadalili ya
vikwazo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment