Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Manda,Oraph Mwinuka akimsikiliza mkuu wa mkoa baada ya kuvuliwa madaraka ya ukuu wa shule.
Mkuu wa mkoa Mh.Ole Sendeka akikagua mradi wa maji kata ya Ludewa Mjini.
Mkuu wa mkoa Mh.Ole Sendeka akikagua mradi wa maji kata ya Ludewa Mjini.
Mkuu wa mkoa Mh.Ole Sendeka akikagua ujenzi wa Dahalia shule ya Sekondari Manda
Mkuu wa mkoa Mh.Ole Sendeka akiwahutubia wananchi wa kata ya Manda
Haya ni madarasa mapya ya shule ya Sekondari Manda
Mkuu wa mkoa Mh.Ole Sendeka akikagua mradi wa maji kata ya Ludewa Mjini.
Mkuu wa mkoa Mh.Ole Sendeka akikagua ujenzi wa madarasa mapya shule ya Sekondari Manda.
Manzari ya shule ya Sekondari Manda wilayani Ludewa
Mkuu wa mkoa Mh.Ole Sendeka akikagua ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya Mlangali wilayani Ludewa.
Mkuu wa Mkoa
wa Njombe Mh.Ole Sendeka amemvua cheo cha ukuu wa shule na kumtaka ahame shule
hiyo mara moja mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Manda Oraph Mwinuka wilayani Ludewa kutokana na
mwalimu huyo kushindwa kusimamia vyema ujenzi wa madarasa, Daharia pamoja na
kushuka kwa ufaulu katika shule hiyo.
Hayo
yamefanyika jana katika ziara ya mkuu wa mkoa,ziara hiyo ambayo inafanyika
katika wilaya Ludewa ikiwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea
kutekelezwa katika maendeo mbalimbali yakiwemo maeneo ya Vituo vya Afya,Shule
na Maji,miradi ambayo imepata fedha kutoka Serikalini.
Mh.Sendeka
alimtaka mwalimu mkuu huyo kukabidhi ofisi kwa makamu wake kutokana na
kushindwa kusimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa katika shule hiyo ikiwa
Serikali imetoa Zaidi ya shilingi milioni mianne kutokea mwaka 2016 lakini
mpaka leo miradi hiyo imekuwa ikisuasua ili hali fedha ipo.
Katika ziara
hiyo Mh.Sendeka alitembelea ujenzi wa majengo mapya ya kituo cha afya cha kata
ya Mlangali ambapo Serikali imepeleka jumla ya shilingi milioni miatano,mradi
wa maji kata ya Ludewa mjini wenye thamani ya shilingi milioni mianne,ujenzi wa
Dahalia,madarasa na nyumba za walimu katika shule ya sekondari Manda wenye
thamani ya Zaidi ya shilingi milioni mianne.
Miradi
mingine ni pamoja na ujenzi wa jingo la upasuaji na majengo mapya ya kituo cha
afya cha kata ya Manda yanayoghalimu kiasi cha shilingi milioni mianne,fedha
hizo zote zimetolewa na Serikali lakini wananchi wanatakiwa kuchangia nguvu zao
ili miradi hiyo ikamilike kwa haraka.
“Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Serikali yake
ametoa fedha za maendeleo ili wananchi waweze kupunguziwa mzigo wa kuchangia
katika ujenzi lakini inashangaza kuona baadhi ya watendaji wa Serikali
wanakwamisha mipango ya Serikali hivyo sitawavumilia watakaojaribu kufanya
hivyo”,alisema Mh.Sendeka.
Mh.Sendeka
pia alifafanua kuhusiana na mpongo wa chakula shuleni kuwa wenye jukumu la
kukusanya chakula na michango yake ni wazazi wenyewe na sio walimu hivyo kauli
ya Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ya elimu
bure na kuzuia michango mashuleni ilikuwa na lengo la kuwapatia nafasi walimu
kubaki katika ufundishaji.
Aidha
aliutaka uongozi wa wilaya ya Ludewa kuwasimamia ipasavyo wakandarasi
wanaojenga miradi mbalimbali wilayani hapa ili iweze kuendana na thamani halisi
ya fedha zinazotolewa na Serikali katika
kuwaletea maendeleo wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment