IGP Sirro akikagua Gwaride mkoani Njombe
MKUU
wa jeshi la polisi nchini,IGP Sirro amewataka wananchi mkoani Njombe
kubadilika mara moja na kuacha mauaji ya imani za kishirikina na ubakaji
katika mkoa huo, kwani mambo hayo hivi sasa yamepitwa na wakati, na
hivyo sheria kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika kwa kuwa jeshi la
polisi limejipanga kudhibiti suala hilo.
“Nimeangalia
uharifu mkoani Njombe upo chini, tatizo kubwa nimeona ni mauaji
yanayotokana na ushirikina, haya mauaji yanaonekana ni mengi, lakini pia
masuala ya kubaka, sambamba na kukamata watu wanaofanya haya mauaji
kazi kubwa tunayoifanya ni kutoa elimu,” alisema IGP Sirro.
Alisema
wananchi waelewe mambo ya ushirikina kwa sasa haya tija, hivyo watu
wanaofanya mauaji kwa ushirikina wengi wamekamatwa, na wamepelekwa
mahakamani huku wakiacha familia zao.
“Wito
wangu katika hilo, watanzania na wana Njombe tubadilike, haya mambo ya
ushirikina yalishapitwa na wakati, ni mambo ya kishamba, tuna kazi ya
kutoa elimu hiyo na nimeelekeza, kamanda na timu yake wajipange vizuri
kwenda kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuzungumzia suala hilo,”
alisema IGP Sirro.
Alisema suala kubwa ni kutoa
elimu kwanza, hivyo akatoa wito kwa viongozi wa dini nchini kuendelea
kutoa elimu kwa mara nyingi watu wanaofanya ushirikina hawana dini, na
hata kama atakuwa na dini, basi atakuwa nayo ya kuhatish
Aidha
kwa hatua nyingine IGP Simon Sirro amewataka Wabunge na wanasiasa
kuacha kuhoji utendaji kazi wa jeshi hilo, na badala yake amewaasa
wananchi kuendelea kusaidia kutoa ushirikiano ili kufanikisha kuwakamata
wahusika.
Akizungumza mara baada ya kukagua
gwaride hilo, IGP Sirro aliwashangaa wanasiasa hususan wabunge akiwemo
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasin kuikosoa kauli yake aliyoitoa akiwa
mkoani Mtwara juu ya Dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
kushindwa kuitikia wito wa kuitwa kuhojiwa na jeshi la polisi ili kutoa
ushirikiano wa upelelezi unaohusiana na tukio la kushambuliwa Lissu
mkoani Dodoma, alisema badala ya kufanya kazi zao kama wanasiasa hivi
sasa wamegeuka kutaka kuanza kukamata watuhumiwa
“Uharifu
kama tumeshindwa kuuzuia kama ulivyotokea, tutahakikisha kwamba kwa
kupata taarifa za wananchi, tunawakamata wahusika,” alisema IGP Sirro.
“Lakini
huyo kijana wao wanayesema tuanze kupeleleza huku, sasa wanatufundisha
kazi, nimeona mbunge mmoja anakaa anasema sijui namna gani, kwa nini
wasianze hivi, naye tumwachie aseme, maana yake ukishakuwa na mdomo ni
lazima aseme, kwa hiyo kimsingi sisi ni professional, tunajua
tunachofanya, hii kazi tumeisomea,” alisisitiza IGP Sirro.
Mkuu
huyo wa Jeshi la Polisi nchini alisema hayo jana mara baada ya kufanya
ziara ya siku moja mkoani Njombe alipotembelea makao makuu ya jeshi la
Polisi mkoani hapa na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na askari
polisi wa jeshi hilo.
“Sasa wanasiasa nao wamekuwa wapolisi
nao wanataka kukamata, wanataka kupeleleza, sasa jamani kazi ya ubunge
imewashinda, mnataka kuwa polisi officer, kwa hiyo watuachie kazi ya
polisi tuifanye kama jeshi la polisi,mambo mengine watuachie sisi,
tunachotaka kwao ni taarifa,” alisema IGP Sirro.
Alisema suala la kuhoji kazi za jeshi hilo, ina maana wanavaa viatu vyake, na pia hawajui jarada la upelelezi limefika wapi.
“Lakini
waelewe kwamba wanafanya siasa kwa sababu kuna amani na utulivu,
tungekuwa tunafanya sisi mambo ya siasa uharifu ungekuwa mkubwa sana
hapa nchini, wala hiyo siasa wasingeifanya, ni waachie wabunge waseme
kwa sababu ni wajibu wao wanapata posho kwa sababu ya kusema,” alisema.
Mwisho
No comments:
Post a Comment