Mkurugenzi wa Shule ya Nicopolis Academy Mwalimu Augustino Mwinuka akichimba shimo la choo cha wanafunzi wakiume shule ya msingi Ludewa mjini.
Mwalimu Augustinio akiwa na vijana wa kikundi cha Ash-tech group wakichimba shimo la choo shule ya msingi Ludewa Mjini.
Mwalimu Augustinio akiwa na vijana wa kikundi cha Ash-tech group wakichimba shimo la choo shule ya msingi Ludewa Mjini.
Baadhi ya wanafunzi wa shule yamsingi Ludewa mjini wakiangalia uchimaji wa shimo la choo chao
Mwalimu mwinuka akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ludewa Mjini
Hiki ndicho choo kinachotumika kwa sasa kikiwa na hali mbaya na tayari kimeshajaa
Madarasa ya shule ya msingi Ludewa Mjini ambayo yalijengwa na hayati Deo Filikunjombe.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule yamsingi Ludewa Mjini iliyoko wilayani Ludewa katika mkoa wa
Njombe Bw.Lazaro Mwinuka ameupongeza
ukongozi wa shule ya watoto ya Nicopolis Academy kwa jitihada zao za kumuenzi
hayati Deo Filikunjombe kwa vitendo.
Akiongea na
mwandishi wa habari hii Bw.Mwinuka alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa vyoo vya wanafunzi na uzio,hivyo wadau
mbalimbali waliosoma shule hiyo waliombwa kuinusuru shule yao lakini mpaka sasa
ni mdau mmoja tu ambaye ni mkurugenzi wa shule ya Nicopolis academy ndiye
aliyejitokeza.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa shule hiyo ambayo inamajengo ya kisasa ambayo yalijengwa na hayati
Filikunjombe lakini imekosa vyoo hivyo uongozi wa Nicopoli Academy umeona uanze
na ujenzi wa vyoo vya wavulana ili kumuenzi hayati Filikunjombe ambaye alikuwa
na mpango wa kuifanya shule hiyo kuwa yakisasa zaidi.
Alisema kuwa
kwa kauli ya Mkurugenzi wa Nicopolis Academy ameanza na uchimbaji wa shimo la
choo hicho lakini anataka kumaliza ujenzi siku ya kumbukumbu ya Deo
Filikunjombe(Deo Filikunjombe Day) ambayo imepangwa kufanyika tarehe 15 oktoba
2017 hivyo ni vyema wadau wengine wakaunga mkono juhudi hizo ambazo zinalenga
maendeleo ya shule hiyo.
“Tunaushukuru
uongozi wa nicopolis academy kwa kuwa tumeona mwanzo mzuri wa kumkumbuka
Filikunjombe kwa vitendo kutokana na enzi za uhai wake alikuwa akishirikiana na
mafundi katika ujenzi wa shule hii na wakati mwingine aliahirisha hata vikao
vya Bunge ili kushiki na mafundi katika kazi hivyo tunawaomba wadau wengine
kufanya haya kwani choo cha wasichana bado ni changamoto”,alisema Bw.Mwinuka.
Akishiriki
na mafundi katika uchimbaji wa shimo la choo hicho Mkurugenzi wa shule ya
Nicopolis Academy Mwalimu Augustino Mwinuka alisema kuwa tayari kazi imeanza
ili kuhitimisha Filikunjombe Day,hivyo wadau wengine wameanza kujitokeza
kumuunga mkono wakiwemo vijana wa kikundi cha ujasiliamali cha Ludewa Ash-tech Group
chenye makao yake makuu Ludewa mjini.
Mwalimu
Mwinuka alisema kuwa ni wajibu wa kila mwanafunzi kuikumbuka shule aliyosoma na
ndiyo maana hayati Filikunjombe aliikumbuka shule hiyo kwa kujenga madarasa ya
kisasa hivyo hata yeye ameanza kwa ujenzi wa vyoo vya kisasa ambavyo vitakuwa
tofauti na shule nyingine wilayani Ludewa.
Alisema kuwa
kama kila mmoja mwenye uwezo wa kafanya jambo japo kidogo katika eneo alilotoka
hasa mashuleni na hospitari basi changamoto zinazowakabili wanaludewe
zitapungua kwani kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya vijana kusahau walikotoka na
kujikita mijini hali ambayo siyo sawa kwa kupitia Filikunjombe Day vijana
wanapaswa kuamka na kukumbuka nyumbani.
Mwisho.
Simu no ya
Mwalimu mwinuka kwa mawalisiano zaidi 0765059184
No comments:
Post a Comment