Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 22, 2017

SHULE YA NICOPOLIS ACADEMY WILAYANI LUDEWA YAWATAKA WALIOSOMA SHULE YA MSINGI LUDEWA MJINI KUMUENZI HAYATI DEO FILIKUNJOMBE KWA MATENDO.

 Mkurugenzi wa shule ya Nicopolis academy Mwalimu Augustino Mwinuka.
Hayati Deo Filikunjombe anzi za uhai wake akifanya kazi ya ujenzi wa Madarasa ya shule ya msingi Ludewa Mjini.



Hayati Deo Filikunjombe anzi za uhai wake akifanya kazi ya ujenzi wa Madarasa ya shule ya msingi Ludewa Mjini.

 Mwalimu Mwinuka pamoja na walimu wenzake wa shule ya Nicopolis Academy wakiwa wanafunzi wa awali wa shule hiyo
 Ujenzi wa Vyoo vya shule ya Nicopolis Academy ukiendelea

 Mwalimu Mwinuka pamoja na walimu wenzake wa shule ya Nicopolis Academy wakiwa wanafunzi wa awali wa shule hiyo
 hizi ni kati ya bembea za watoto katika shule hiyo.


 Mwalimu Mwinuka akiwa na wanafunzi wa pre form one katika shule ya Nicopolis Academy

Hayati Deo Filikunjombe anzi za uhai wake akifanya kazi ya ujenzi wa Madarasa ya shule ya msingi Ludewa Mjini.


Mkurugenzi wa shule ya watoto ya NICOPOLIS ACADEMY  iliyoko wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe Mwalimu Augustino Mwinuka  amewataka wadau mbalimbali waliosoma shule ya msingi Ludewa Mjini kumuenzi hayati Deo Filikunjombe kwa matendo hasa katika kujitolea kuiboresha shule hiyo.

Akiongea na wanahabari Jana ofisini kwake Mwalimu Mwinuka alisema kuwa tarehe 15/10/2017 ni siku pekee iliyopangwa kifamilia kumuenzi hayati Filikunjombe hivyo kama mdau wa elimu atafanya baadhi ya matendo yakimaendeleo yaliyokuwa yakifanywa na hayati Filikunjombe ikiwa pamoja na ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Ludewa mjini.


Mwalimu Mwinuka alisema Kuwa Hayati Filikunjombe alikuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo katika wilaya ya Ludewa hivyo ameacha alama kubwa pale alipoamua kujenga madarasa ya kisasa katika shule ambayo alisoma elimu ya msingi inayojulikana kwajina la Shule ya msingi Ludewa mjini.


Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa kuna watu wamefanikiwa kimaisha kupitia shule hiyo lakini wameshindwa kuja kumuunga mkono hayati Filikunjombe kwa kile alichokianzisha hivyo ni wajibu wa kila mmoja aliyesoma katika shule hiyo kuunga mkono juhudi hizo kwani shule hiyo ni kioo cha wilaya ya Ludewa lakini inachangamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa vyoo vya kisasa pamoja na kukosa uzio ili kuweka usalama wa wanafunzi.


“Mimi sina kipato kikubwa lakini kupitia ada ninazokusanya katika shule yangu ya Nicopolis Academy japo bado changa nitaziunga mkono juhudi za hayati Filikunjombe kwa kujenga choo cha kisasa cha wanafunzi wa kiume kwa kuwa na mimi nilisoma shule hii,kazi hiyo naianza sasa na natarajia kuhitimisha siku ya kumbukumbu yake,hivyo nawaomba wale wote tuliosoma katika shule hii tuungane kutatua baadhi ya changamoto za shule yetu”,alisema Mwalimu Mwinuka.


Mwalimu Mwinuka alisema kuwa kwa wale waliosoma katika shule ya msingi Ludewa mjini ni wajibu wao lakini aliwataka wadau mbalimbali,ndugu,jamaa na Marafiki wa hayati Deo Filikunjombe wanaotambua umuhimu wa elimu na waliokuwa wakizikubali kazi zake kuunga mkono juhudi hizo ili kumuenzi kwa vitendo na sio kwa maneno.


Alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakipongeza kazi za Hayati Filikunjombe kwa maneno wawapo mitaani lakini wanasahau kupongeza kazi hizo kwa matendo hivyo wakati umefika sasa wa kumpongeza kwa matendo na sio maneno tena kwa yeyote anayefanya mazuri anastahili pongezi kwa vitendo .


Aidha aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kuungana naye siku ya kilele cha kumbukumbu ya Filikunjombe katika ujenzi wa vyoo hivyo kutokana na ukweli kwamba madarasa yaliyojengwa na hayati Filikunjombe katika Shule hiyo ni ya kisasa na yanahitaji mwendelezo wa wadau wa elimu katika changamoto zile ndogondogo zilizosalia.


Wanaotaka kumuunga mkono Mwalimu Mwinuka,piga simu 0765059184.

Mwisho.

No comments: