Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna Warioba,
ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake
kuacha tabia hiyo mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji
umesababisha kifo.
Kamanda
Shanna amelazimika kusema hayo hayo wakati akitolea ufafanuzi juu ya
tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji cha Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma
Habibu ( 26).
Kwa
mujibu wa Shanna Marehemu aliuwawa juzi majira ya saa mbili asubuhi
wakati walipokuwa kijiweni na wenzake baada ya kutokea ugomvi kati yake
na Ramadhani Habibu (23) ambaye ni ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja
ambaye anadaiwa kuwa na maumbile makubwa (makalio) kupita, mbele yao.
Alisema
baada ya mwanamke huyo kupita mbele yao walianza mabishano ambapo
marehemu alisema mwanamke huyo ana makalio makubwa na Ramadhani alisema
ni makalio ya kawaida sio makubwa.
Kamanda
Shanna alieleza kuwa baada ya mabishano hayo ndipo ulipozuka ugomvi
hadi kufikia hatua ya Ramadhani kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu
kifuani upande wa kuliana na alifariki dunia akiwa njiani anapelekwa
hosptali ya kisarawe.
Alisema
jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kuwa
atafikishwa mahakamani mara moja na kuwa amekubali kuwa amefanya
mauaji hayo.
Kufuatia,tukio
hilo kamanda Shanna aliendelea kutoa onyo kwa wananchi na vijana
wanaoshinda vijiweni kuacha tabia ya udhalilishaji hasa kwa wanawake na
kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwa kama kuna mtu aliyefanyiwa
vitendo vya namna hiyo atoe taarifa polisi na atafikishwa mahakamani.
"Wito
kwa wale wanaokiuka haki za binadamu kwa kumdhalilisha mtu waache mara
moja, mfano kisheria hata kumkonyeza mtu ni kosa la jinai hivyo unapaswa
kufika polisi, na tutamfuatilia kisha kumpeleka mahakamani" Kamanda
Shana amefafanua
Pia kamanda Shanna ametoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao ili kuepusha vishawishi na matamanio kwa wanaume
No comments:
Post a Comment