Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

January 30, 2017

ZIARA YA WAZIRI MKUU MH KASSIM MAJALIWA WILAYA YA LUDEWA YAWA MWIBA KWA WAPIGA DILI.

Waziri Mkuu Mh.Majaliwa  akitembea kwa miguu kupandisha mlima wenye madini ya chuma katika kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa
 Hii ni ramani ya viwanda vya kuchakata chuma vitakavyojengwa  eneo la kata ya Mundindi


Viongozi mbalimbali wakisubiri kusalimiana na Waziri mkuu Mh.Majaliwa

Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiwa katika eneo lenye madini ya Chuma





Wananchi wilayani Ludewa wamempongeza waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa kwa kufanya ziara wilayani Ludewa na kuweka bayana kuhusiana na ulipwaji Fidia kwa baadhi ya wananchi wanaotakiwa kuhama maeneo ya machimbo ya chuma na makaa ya mawe.

Akizungumza na wanahabari mmoja wa wananchi hao wa kijiji cha Mundindi ambako ndiko kwenye madini ya chuma BW.Simon Mgina alisema kuwa alichokifanya waziri mkuu kutembelea eneo hilo na kuwaeleza bayana wananchi kuwa kuna baadhi ya wapiga dili wanataka kunufaika kupitia migongo ya wananchi wa eneo hilo imezua minong’ono vijiweni.

Bw.Mgina alisema kuwa tayari wananchi wameanza kutambua ukweli kwa nini ulipwaji wa fidia hizo umechelewa tofauti na awali wananchi hao walikuwa wakiitupia lawama Serikali kwa kuchelewesha ulipwaji wa fidia hiyo.

Alisema taarifa hii ya kuwa baadhi ya watu wanataka kutembelea migongo ya wananchi wanyonge imewashtua wengi na tayari baadhi ya watu wameanza kupiga simu kwa ndugu zao walioko mbali na eneo hilo kuwa hali imebadirika na kama walikubariana na wathaminishaji kuwa wakipata kiasi Fulani kitarudi kwa wathaminishaji hilo jambo wasahau.

“Tumeanza kuona baadhi ya ndugu zetu hapa kijijini wakiwasiliana na ndugu zao walioko mijini na kuwaeleza hali halisi ili kama kunamipango iliandaliwa basi itakuwa imeshindikana kwani awali kulikuwa na tambo nyingi vilabuni kuwa watalipwa fedha nyingi lakini kwa sasa wamekuwa wapole huwezi kuamini”,alisema Bw.Mgina.

Katika ziara ya waziri mkuu Mh.Majaliwa wilayani Ludewa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mundindi na Ludewa mjini alisema kuwa Fedha ya kulipa fidia imeshatengwa na ipo tayari kiasi cha 13 Bilioni lakini Serikali inataka kujiridhisha katika mikataba ya wawekezaji na Serikali ili kuona kama itakuwa na manufaa kwa Taifa.

Mh.Majaliwa alisema kuwa Serikali imeshituka jambo baada ya kuona bajeti ya Fidia ni kubwa sana tofauti na uhalisia hiyo aliwataka wananchi kuwa wapole wakisubiri Serikali kuhakiki ulipwaji wa fidia hiyo kabla ya kulipa kwani wamebaini kuwa kuna wajanja wanataka kunufaika kupitia migongo ya wanyonge.

Mwisho.

No comments: