Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

January 30, 2017

MDAU WA SOKA WILAYANI LUDEWA CREDO FILIKUNJOMBE AWAUNGA MKONO VIJANA.

 Credo Filikunjombe akimkabidhi mipira mipira miwili mwenyekiti wa kijini Bw.Kayombo
Bw.Credo akiongea na wachezaji wanaoshiriki ligi hiyo ya kijiji cha Lupingu


 Bw.Credo akiongea na wachezaji wanaoshiriki ligi hiyo ya kijiji cha Lupingu
 Msimamizi wa mashindano hayo Bw.Joseph Mpolo akiongea na wachezaji

  Bw.Credo akiongea na wachezaji wanaoshiriki ligi hiyo ya kijiji cha Lupingu
Huu ndio mpira wa awali ulipasuka katikati ya pambano ambao ulikuwa mpira wa mikono ulishindwa kumaliza pambano la mpira wa miguu lakini ukiwa ni mpira wa tatu kupasuka uwanjani.




Mdau wa soka wilayani Ludewa na mjumbe wa mkutano mkuu ccm Taifa kupitia wilaya ya Njombe Bw.Credo Filikunjombe ambaye pia ni mwalimu wa mpira wa miguu amewaunga mkono vijana wa kijiji cha Lupingu wilayani hapa kwa kuwapatia vifaa vya michezo.


Akikabidhi viafaa hivyo vya michezo ambayo ni mipira miwili kwa mwenyekiti wa kijiji cha Lupingu Bw.Credo alisema kuwa amefikia uamuzi huo wa kununua mipira hiyo kutokana na uhaba mkubwa unaozikabiri timu za kijiji hicho ambacho kinafanya mashindano ya kijiji yanayozishirikisha timu nne.


Bw.Credo ambaye ni mdogo wa liyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa Hayati Deo Filikunjombe alisema kuwa ligi hiyo ya kijiji imekuwa ni ligi yenye upinzani mkubwa lakini mara nyingi michezo yake imekuwa ikiishia njiani kutokana na kukosekana kwa mipira ya kuchezea kwani wamekuwa wakiazima mipira vijiji jirani na wakati mwingine walichezea mpira wa mikono ambao ulishindwa kumaliza pambano na kupasuka katikati ya mchezo.


Alisema kuwa kutokana na udau wake katika michezo pia mafunzo aliyoyapata TFF mwaka 2005 ya ualimu wa mpira wa miguu mjini Iringa imemlazimu kununua mipira hiyo kwa pesa yake na kumkabidhi mwenyekiti wa kijiji ili kuendeleza vipaji kijijini hapo na kumaliza tatizo la ukosefu wa mipira ya kuendeshea ligi hiyo ya kijiji cha Lupingu.


‘’mimi kama mdau wa michezo na usafiri wangu unafanya safari za huku nimeona ni vyema kuwaunga mkono walioanzisha ligi hii ambao ni kijiji cha Lupingu kwa kutoa mipira hii lakini nawaomba vijana kutunza vifaa hivi kwani kunabaadhi ya vijana sio waaminifu wamekuwa wakipewa vifaa vya michezo lakini kutokana na tamaa zao za fedha huviuza’’,alisema Bw.Credo.


Alisema kuwa tayari kuna malalamiko miongoni mwa vijana hao kuwa baadhi yao wakiaminika kama viongozi wa timu ya kijiji walipewa jezi na mbunge wa jimbo la Ludewa Mh Ngalawa lakini wamegawana na kuzivaa mitaani na kuifanya timu yao kuazima jezi kijiji cha Ntumbati wakati jezi za Ludewa kwanza zililetwa.


Akipokea msaada huo mwenyekiti wa kijiji cha Lupingu Bw.Kayombo alisema kuwa lengo la kuanzisha ligi hiyo ni kukuza vipaji vya vijana na kuchagua wachezaji wa timu ya kijiji lakini ligi hiyo imekuwa ikisuasua kutokana na ukosefu wa mipira ya kuchezea hivyo alimpongeza Bw.Credo kwa moyo wake wa kujitolea mipira hiyo.


Aidha Bw.Kayombo amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitatuzwa katika ofisi ya kijiji kutokana na ukweli kwamba viongozi wa kata akiwepo diwani wa kata ya Lupingu pia Mbunge wa jimbo la Ludewa walitoa vifaa vya michezo na kuwakabidhi viongozi wa timu lakini mpaka sasa hakuna hata kifaa kimoja na inasadikika vimeuzwa pia aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia vifaa vya michenzo katika kijiji cha Lupingu na kata nzima ili kukuza vipaji kwa vijana.


Mwisho.

No comments: