Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

December 06, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA MH.DEO NGALAWA AWATAKA WANANCHI LUDEWA KUWAKARIBISHA WAWEKEZAJI.

Katibu wa jimbo la Ludewa Bw.Fortunatus Fungatwende akiongea na wazazi wenye watoto katika shule ya watoto wadogo Morning Star.
Mkurugenzi wa shule ya Morning Star Bw.Maulid Mwingira akiongea katika mahafari hayo


wanafunzi wa Morning star wakiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja
 wanafunzi wa Morning star wakiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja
Bw.Fungatwende akikagua mabweni ya Mornig stara
 Bw.Fungatwende akitoa vyeti kwa wahitimu
Baadhi ya wazazi wakifurahi na watoto wao baada ya kuhitimu elimu ya awali katika shule ya Morning star
Bw.Fungatwende akikagua maktaba ya Morning star
Baadhi ya wazazi wakifurahi na watoto wao baada ya kuhitimu elimu ya awali katika shule ya Morning star
 wanafunzi wa Morning star wakiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja




Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh.Deo Ngalawa amewataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kuwakarimu wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika wilaya hii ili kuweza kufungua mianya ya kibiashara baina ya wageni na wenyeji kwani kwa kufanya hivyo vijana wanaweza kujipatia vipato.

Akiongea katika mahafari ya pili ya shule ya watoto ya Morning star iliyoko wilayani hapa mtaa wa mdonga katibu wa mbunge huyo Bw.Fortunatus Fungatwende kwa niaba ya Mh.Ngalawa ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi Bw.Fungatwende alisema kuwa kumekuwa na urasimu kwa wawekezaji kushindwa kufanya kazi zao kwa uhuru kutokana na baadhi ya wananchi na viongozi wa Serikali kutotengeneza mazingira rafiki.

Bw.Fungatwende alisema kuwa inashangaza kuona baadhi ya wadau wenye lengo la kuwekeza Ludewa wanashindwa kufanya hivyo kutokana na vikwazo kutoka kwa wananchi na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwani hushinikiza mambo yasiyo na tija kwa maendeleo ya wilaya ya Ludewa.

Alisema kuwa wilaya ya Ludewa inatakiwa kufungua mipaka ili wawekezaji wawekeze kwa wingi katika ujenzi wa shule,Hospitari na vyuo ili kuifanya wilaya kuwa na watu wengi wa makabila tofauti tofauti ambapo kwa kufanya hivyo kutakuwa na mzunguko mkubwa wa kifedha na sio kuwawekea vikwazo wawekezaji kwa kuwapandishia gharama za Ardhi na bei kubwa ya vifaa vya ujenzi.

“tunamshukuru mkurugenzi wa shule hii ya Morning star kwa kuwekeza Ludewa kwani yeye siyo mwanaludewa lakini ameamua kuwekeza katika sekta ya elimu ili watoto wetu waweze kupata elimu richa ya kuwa alikutana na vikwazo vingi hivyo nawaomba wananchi na viongozi wa halmashauri kushirikiana na wawekezaji wa sekta binafsi ili kuleta maendeleo ya kweli Ludewa na sio kuwawekea vikwazo visivyo vya msingi”,alisema Bw.Fungatwende.

Aidha Mkuregenzi mtendaji wa shule ya watoto ya Morning star Bw.Maulid Mwingila alimshukuru mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Ngalawa kukubari kuwa mgeni rasmi katika mahafari ya shule yake pia alimsifu kwa kuliona jambo la ugumu unaowakuta wanaotaka kuwekeza wilaya ya Ludewa kutokana na kupanda kwa gharama za Ardhi hasa kwa wageni.

Bw.Mwingira alisema kuwa mpango wa Morning star ni mkubwa kwani awali viliibuka vikwazo vingi mno ila kutokana na roho ya ujasiri waliweza kuvishinda vikwazo hivyo na ujenzi ukaendelea na mpaka sasa shule hiyo inaendelea vizuri na inawanafunzi wa kutosha hivyo aliwataka wazazi wilayani hapa kuwarithisha watoto wao elimu badala ya mashamba na Ng’ombe.

Mwisho.

No comments: