wananchi wa Shaurimoyo wilayani Ludewa wakikubaliana jambo la kutolipwa fidia na mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Tsere.
Mhandishi Sanyiel Kishimbo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Herkin Builders LTD akisaini mkataba wa ujenzi wa chuo cha VETA kijiji cha Shaurimoyo
Ramani ya chuo cha Veta Shaurimoyo
Mhandishi Sanyiel Kishimbo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Herkin Builders LTD akikabidhiwa mkataba wake kwa Mhandishi mshauri wa VETA
Mhandisi Suzani ambaye anasimamia kata ya nyanda za juu kusini akisaini mkataba
Hivi ndivyo sura ya chuo cha veta Shaurimoyo kitakavyokuwepo
Katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Fungatwende akiongea na wananchi wa shaurimoyo
Mhandishi Sanyiel Kishimbo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Herkin Builders LTD akiongea na wananchi wa kijiji cha Shaurimoyo katika wilaya ya Ludewa.
Serikali
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kupitia wataalam wa VETA Taifa imeingia
mkataba rasmi jana na mkandarasi ambaye ni HERKIN BUILDERS LTD kutoka jijini
Dar es Salaam ili kufanikisha ujenzi wa chuo cha VETA cha mkoa wa Njombe kinachojengwa
wilayani Ludewa katika kijiji cha Shaurimoyo kata ya Lugarawa.
Akitoa
ufafanuzi kuhusiana na ujenzi wa chuo hicho mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Andrea
Tsere alisema kuwa ni heshima ya pekee ambayo wilaya ya Ludewa imepewa kujengwa
chuo chenye hadhi ya mkoa ikiwa ni ilani ya chama cha mapinduzi ya Serikali ya
awamu ya tano.
Mh.Tsere
alisema chuo hicho cha VETA kitagharimu kiasi cha shilingi 9.8 bilion kwa
makisio ya awali pia chuo hicho kitatoa kozi ambazo zitaendana na mahitaji ya
migodi mikubwa miwili inayotarajia kuanza hivi karibuni ya mchuchuma kule Nkomang’ombe
na chuma cha Liganga ambapo wanafunzi watakaohitimu chuo hicho na kufaulu
vizuri wanauwezekano mkubwa wa kuajiriwa katika migodi hiyo.
Aliwataka
wananchi wa Shaurimoyo kuonesha ushirikiano mkubwa kwa mkandarasi aliyepewa
kazi hiyo ili aweze kuifanya kazi hiyo kwa haraka pia alimtaka mkandarasi huyo
kutoa ajira zaidi kwa vijana wa wilaya ya Ludewa ili kuongeza kipato kwa
wanaludewa kwani kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wakandarasi kutoka na
vibarua pia mafundi maeneo mengine na kuacha wenyeji wakiwa watazamaji tu.
“Nakuagiza
mkandarasi kuangalia nafari za kazi katika ujenzi wa chuo hiki kwani tunavija
wetu hapa hawanakazi nahii ni fulsa kwao
kupata kazi za vibarua pia mafundi ujenzi wako hapa,kumekuwa na tabia ya baadhi
ya wakandarasi kusafiri na wafanyakazi pamoja na vibarua kutoka maeneo mengine
na kuwaacha wenyeji wakiwa watazamaji,jambo hilo hapa kwetu hatutaki litokee”,alisema
Mh.Tsere.
Aidha Mkurugenzi
wa kampuni ya Herkin Builders LTD Mhandishi Sanyiel Kishimbo alisema kuwa
mkataba alioingia na Serikali ni mzuri kwani ujenzi utaanza rasmi tarehe 9
January 2017 na ataikabidhi funguo za Chuo tarehe 25 August 2017 kusipotokea
tatizo lolote hivyo aliwataka viongozi wa Serikali na wananchi kumpatia
ushirikiano ili kufanikisha ujenzi huo.
Mhandishi
Kishimbo alisema kuwa richa ya kuwa na changamoto ya usafirishaji wa vifaa
lakini Serikali imempatia muda wa siku 28 kusogeza vifaa vya ujenzi katika eneo
la mradi hivyo vijana wanapaswa kujiandaa na fulsa ya ajira kama alivyosema
mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Andrea Tsere.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment