mabango wa wananchi wa Nkomang'ombe
mabango wa wananchi wa Nkomang'ombe
Wananchi wa Mundindi katika mradi wa chuma wakiwa na mabango yao
Wananchi wa Mundindi katika mradi wa chuma wakiwa na mabango yao
Mwenyekiti wa Bodi ya NDC Taifa Dr.Samwel Nyantahe mwenye shati nyeupe akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Edward Haule katika maabara ya Makaa ya mawe Nkomang'ombe
Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr.Nyantahe akiwa na Viongozi mbalimabali katika mradi wa chuma Liganga
Dr.Nyantahe akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa MMI kuhusiana na uchimbaji wa chuma
Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr.Nyantahe akiwa na Viongozi mbalimabali wakiwemo maofisa kutoka ofisi ya mbunge wa jimbo la Ludewa katika mradi wa Makaa ya mawe Nchuchuma
Dr.Samwel Nyantahe akiongea na mwandishi wa mtandao huu Nickson Mahundi
Dr.Nyantahe akiwa na mwandishi na mmilikiwa mtandao huu Bw.Nickson Mahundi
Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr.Nyantahe akiwa na Viongozi mbalimabali katika mradi wa chuma Liganga
Dr.Nyantahe akionesha jiwe la chuma kwa waandishi wa habari
Dr.Nyantahe akiwa na mwandishi na mmilikiwa mtandao huu Bw.Nickson Mahundi
Mwenyekiti
mpya wa Bodi ya Shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Dr.Samuel Nyantahe
amepokelewa kwa mabango yenye jumbe nzito wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
kuashiria kukelwa na ahadi za Serikali ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara
na viongozi wa shirika hilo kuhusiana na ulipaji wa fidia katika maeneo yao.
Wakiongea
kwa jazba jana wakati uongozi wa NDC ulipotembelea maeneo ya migodi ya Makaa ya
mawe Nchuchuma na chuma cha Liganga katika kata ya Mundindi kwa lengo la
kumuonesha Mwenyekiti huyo fulsa zilizopo maeneo hayo ili Serikali iendelee na
utaratibu wa uwekezaji walisema kuwa wamechoshwa kuona viongozi wakifika maeneo
hayo bila kutoa jibu la fidia ili kupisha uwekezaji italipwa lini.
Mmoja wa
wananchi hao Bi.Angelina Mgeni mkazi wa kata ya Mundindi wilayani Ludewa alisema
kuwa eneo ambalo zimejengwa kambi za wachina ambao ni wawekezaji wa miradi hiyo
ndipo yalipokuwa makazi yao tokea akiwa mtoto mdogo lakini mpaka wazazi wake
walifariki na kuzikwa eneo hilo alikuwa akisikia kutakuwa na uchimbaji wa chuma
lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.
Bi.Angelina
alisema kuwa NDC waliwatoa eneo hilo ili kupisha wawekezaji na wakiahidiwa
watalipwa fidia lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea hivyo ifikapo tarehe
moja Januari 2017 kama hakuna malipo atarudi kupanda miti eneo lao la Familia
bila kujari kuna nyumba za raia wakichina maana wameshindwa kufanya shughuri za
kimaendeleo kwa muda mrefu na hivyo kuwafanya uchumi wao kudorola.
“nimezaliwa
katika eneo hili na hata wazazi wangu wamezikwa katika mashamba haya ambayo kwa
sasa ni kambi za wachina na baadae tukaamuliwa kuondoka eneo hili ili kupisha
wawekezaji lakini tuliahidiwa kulipwa fidia ili tukatafute mashamba katika
maeneo mengine na uthamini ulishafanyika na tukaelezwa tungelipwa tarehe moja julay
mwaka huu lakini hakuna kinachoendelea,ikifika January mwaka ujao nitarudi
kupanda miti katika eneo langu nimechoka kudanganywa”,alisema Bi.Angelina.
Wananchi hao
walisema kuwa kijiji cha Mundindi kimekuwa nyuma kimaendeleo tofauti na vijiji
vingine wilayani Ludewa kutokana na ahadi za shirika la maendeleo la Taifa
(NDC)kuwazuia kuendeleza maeneo yao ili uwekezaji wa migodi hiyo uweze
kufanyika lakini ahadi hizo zimekuwa hewa hali ambayo wananchi wanahitaji
kurudishiwa Ardhi yao ili waendelee na uzalishaji mali.
Akijibu
jumbe mbalimbali zilizoandikwa katika mabango zikiambatana na maswali mengi
kutoka kwa wananchi Mwenyekiti wa bodi ya NDC Taifa Dr.Samwel Nyantahe alisema
kuwa ni kweli wananchi ni haki yao kulalamika lakini wanatakiwa kuwa na subira
kwani Serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda hivyo yeye ni mwenyekiti mpya wa
bodi hiyo na alifanya ziara hiyo ili kujiridhisha na uwepo wa utajiri huo.
Dr.Nyantahe
alisema kuwa tayari fedha za ulipaji wa fidia zimeshatengwa na kilichokuwa
kikifanyika ni kupitia upya mikataba hiyo na wawekezaji zoezi ambalo tayari
limekwisha na hatua ya mwisho ni kupitishwa katika baraza la Mawaziri ili
kubariki ulipaji huo uendelee hivyo wananchi wanatakiwa kupunguza jazba na
kuiamini Serikali yao katika utekelezaji.
Aidha
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni diwani wa kata ya
Ibumi kupitia chama cha mapinduzi Mh.Edward Haule alimuomba mweyekiti huyo wa
Bodi kuhakikisha majibu sahihi ya lini fidia inalipwa kwa wananchi hao kwani
imekuwa ni kero kubwa kwa viongozi wa Serikali kutembelea katika kata hizo na
kuongea na wananchi.
Mh.Haule
alisema kuwa wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakiitumia ardhi hiyo katika
kujizalishia mali na kujipatia kipato ambacho kimekuwa ni msaada katika familia
zao kama ulipaji wa ada za familia mashuleni lakini kwa kuzuiliwa kwa muda
mrefu kutolima mazao ya kudumu katika maeneo hayo kumewarudisha nyuma katika
maendeleo wakisubiri fidia ili wakanunue mashamba maeneo mengine.
Alisema kila
viongozi wa ngazi ya wilaya wanapopanga ziara ya kuwatembelea wananchi hao
mikutano huvurugika kutokana na hasira walizonazo wananchi hao katika kulipwa
fidia zao hivyo kama kiongozi mkuu wa bodi ya NDC anapaswa kulitazama kwa
umakini mkubwa jambo hilo ili kuleta amani baina ya viongozi wa kiserikali na
wananchi hao katika kuleta maendeleo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment