Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

February 06, 2013

SHEREHE YA SIKU YA SHERIA DUNIANI YAFANA WILAYANI LUDEWA


Hakimu mfawidhi mkazi wa wilaya ya Ludewa Mh.Fredrick Lukuna akifungua siku ya sheria duniani iliyoazimishwa kiwilaya katika viwanja vya Mahakama ya wilaya Ludewa
Viongozi mbalimbali wakisikiliza maelezo ya awali kuhusiana na umuhimu wa sherehe hizo
 Mh.Lukuna akifurahi jambo na katibu tawala wa wilaya ya Ludewa Bw.John Mahali
 Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akikaribishwa na mwenyeji wake Mh.Lukuna ambaye ni hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Ludewa katika sherehe za siku ya sheria
 kiongozi wa dini akisoma Dua katika sherehe hizo
Bw,Jose Kamonga mwanasheria alihudhuria sherehe hizo wilayani Ludewa
 Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Mdaha akitoa hotuba kwa wananchi
 viongozi wa dini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi
 Mh.Lukuna na Mkuu wa wilaya ya Ludewa wakielekea katika jikwaa la sherehe ya siku ya sheria Duniani iliyoadhimishwa kiwilaya katika viwanja vya mahakama ya wilaya Ludewa
kiongozi wa dini akisoma Dua katika sherehe hizo 
 Katibu tawala wa wilaya ya Ludewa Bw.John Mhali akiwasalimia wananchi

 Kikundi cha ngwaya cha mpangwa kikisherehesha sherehe hiyo
 wananchi wa wilaya ya Ludewa wakiwa katika sherehe za siku ya sheria Duniani katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya Ludewa.
 Wafanyakazi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja
Hakimu wa wilaya ya Ludewa Mh.Fredrick Lukuna



Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma madaha akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa katika picha ya pamoja katika viwanja vya mahakama hiyo.
Waandaaji wa chakula kutoka Mgahawa wa Mama Mudy wakiwa katika sale ya pamoja tayari kuhudumia wageni mbalimbali waliofika katika sherehe hizo
 Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akifurahi jambo na Mh.Lukuna
 Viongozi wa dini mbalimbali wakijumuika katika chakula siku ya sheria Duniani
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akipata chakula
wafanyakazi wa nahakama ya wilaya ya Ludewa na wageni waalikwa wakipata chakula katika sherehe hizo
Askari akionyesha vidhibiti alivyokamatwa navyo mtuhumiwa katika sherehe hizo za siku ya sheria
Mtuhumiwa akisomewa mashitaka yake katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya ya Ludewa
Askari wa jeshi la polisi ndio ambao wasimamizi wakuu wa sheria wakiwa katika sherehe hiyo.
Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ludewa
Hakimu Mh.Lukuna akifurahi jambo katika sherehe hizo
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akiwa na viongozi mbalimbali

WATENDAJI WA MITAA,VIJII WAASWA KUTOJIFANYA MIUNGU WATU KATIKA JAMII WANAZOZIONGOZA

WATENDAJI wa mitaa na vijiji nchini wametakiwa kutojichukulia sheria mikononi na kuonekana wao ni miungu watu katika maeneo yao ya kazi kwa kile kinachodaiwa kuwanyanyasa wananchi katika maamuzi ya kesi mbalimbali na badala yake wawashauri wananchi hayo kufungua kesi mahakamani.

Hayo yalisemwa leo na mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha katika sherehe ya Sheria Duniani ambazo huadhimishwa Februal 6 kila mwaka ambapo aliwataka watendaji hao kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa kutunga sheria zao kandamizi.

Bw.Madaha alisema imefikia wakati watanzania wanaichukia Serikali yao kutokana na sheria ndogondogo zinazotungwa na watendaji hao hali ambayo huwafanya wananchi kuona Serikali ndio inayowanyanyasa wakati hakuna suala kama hilo.

Alisema watanzania walio wengi bado hawajui sheria hivyo kutokujua kwao sheria ndio husababisha wanyanyaswe kwa kuhukumiwa kutoa fedha katika makosa yasiyo ya msingi hivyo kama kesi hizo zinazoamuliwa na watendaji zitafikishwa katika mahakama za mwazo basi usawa wa kisheria utatendeka ipasavyo.

“Napenda kuwaelaza watendaji wa vijiji na mitaa wanaotaka kuonekana miungu watu waache mara moja kwani wananchi wanailalamikia Serikali yao kwa kuto watendea haki wakati kuna watendaji wachache wasio waadirifu huwatisha wananchi kwa kuwahukumu visivyo hali ambayo inapelekea kupenyeza mianya ya Rushwa huko vijijini”,alisema Bw.Madaha.

Bw.Madaha alisema kumekuwa na tabia ya watendaji hao kutaka kuogopwa na wananchi na kuwachangisha michango isiyo na msingi wowote hali ambayo hupelekea asiyetoa hukamatwa na kufungiwa maofisini na wakati mwingine hutumwa mgambo kukamata mifugo yake na kuuzwa kwa kufidia michango.

Alisema kitendo hicho na vitendo vingine vya unyanyasaji wa wananchi havifai kwani vinaashilia uvunjifu wa sheria zilizopangwa na Serikali hivyo wananchi wanaweza kuichukia Serikali yao na kujiona wakiishi kama wakimbizi kutokana na manyanyaso wanayoyapata kwa baadhi ya watendaji.

Aidha Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Ludewa Mh.Fredrick Lukuna akisoma risala mbele ya mgeni rasmi alisema kaulimbiu ya sherehe hiyo ni utawala wa sheria,umuhimu na uimarishwaji wake nchini na kila nchi ya kidemokrasia huongwazwa na katiba ambayo huchukuliwa kama mama wa nchi husika.

Bw.Lukuna alisema kila mwananchi huheshimu na kutii katiba,sambamba na hayo sheria zote zinazotungwa na Bunge lazima zitii katiba iliyopo pia majukumu muhimu ambayo Dola inatakiwa kutekeleza katika kuzingatia utawala bora ni kuhakikisha amani na usalama wa watu na Taifa vinaonekana  na kufanyiwa kazi ipasavyo.

Alisema Tanzania ni nchi mojawapo kati ya nchi zinazofuata utawala wa sheria na hayo yote katika utunzwaji wa haki za binadamu yanajidhihilisha katika ibara ya 13 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inayosema”Watu wote ni sawa mbele ya sheria,na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote,kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria”.

Bw.Lukuna alisema katiba ibara ya 107A inatamka bayana kuwa mamlaka yanye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania itakuwa ni Mahakama katika kutenda haki kwa wote bila kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi.

Kama hayo yatatekelezwa na watendaji wa viviji,mitaa na watumishi wa Mahakama basi utawala wa sheria na umuhimu wake utaonekana katika jamii yetu hivyo cha muhimu katika nchi ya kidemokrasia inayofuata dhana ya utawala bora lazima Mahakama iwe huru katika kutoa maamuzi yake na siyo kuingiliwa na chombo chohote cha utawala.

Mwisho.

No comments: