Kaimu mganga mkuu wa hospitari ya wilaya ya Ludewa Dkt.Frank Mwambasanga
wodi ya watoto katika hospitari ya wilaya ya Ludewa
Kituo cha
watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi wilayani Ludewa katika mkoa
wa Njombe kimetoa misaada mbalimbali kwa watoto wenzao ambao ni wagonjwa na
wamelazwa katika wodi ya watoto hospitari ya wilaya ya Ludewa.
Akitoa
msaada wa Sabuni na vitu vingine jana kwa watoto waliolazwa katika hospitari hiyo
Mkurugenzi wa NICO POLIC ACADEMY Bw.Augustino Mwinuka alisema kuwa lengo la
kwenda na watoto wa kituo hicho ili kuwajulia hali watoto wagonjwa waliolazwa
katika hospitari ya wilaya ya Ludewa ni kuwafundisha watoto wa NICO POLIS
ACADEMY kuwa na matendo ya huruma.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanatakiwa kujifunza
upendo kwa kuonesha watoto wengine hivyo ni utaratibu wa kituo hicho
kuwatembeza watoto hao katika kuisaidia jamii nyingine yenye shida zaidi ya
watoto wanaotoka NICOPOLIS ACADEMY.
Alisema kuwa
kituo hicho kinachukua watoto wa aina mbalimbali ambao ni watoto wenye ulemavu
wangozi,watoto yatima na wanaoishi mazingira hatarishi pia baadhi ya wazazi
huwaleta watoto wao ili waweze kupata elimu kwa kuchangia gharama nafuu.
“Tumewaleta
watoto hawa kuwaona watoto wenzao ambao ni wagonjwa na kuwapatia vitu vichache
ili kuwafundisha watoto tulionao katika kituo chetu waweze kuwa na moyo wa
huruma na kuwajali wengine kwani watoto wengine tulio nao wameharibiwa
kisaikolojia kutokana na maisha waliokuwa wakiishi kabla ya kuja kuishi katika
kituo chetu hivyo inaweza kusaidia kuwaweka sawa katika jamii”,alisema
Bw.Mwinuka.
Akitoa
shukrani zake kwa uongozi wa kituo cha NICO POLIC ACADEMY kaimu mganga mkuu wa Hospitari ya wilaya ya
Ludewa Daktari.Frank Mwambasanga alisema kuwa kituo hicho ni mfano wakuigwa
kwani wameonesha kuwa wapo kwaajili ya jamii na si vinginevyo.
Dkt.Mwambasanga
alisema kuwa kituo hicho kimetoa faraja kwa watoto hao ambao ni wagonjwa richa
ya kuwa wamekuja kuwafundisha watoto wanaoishi kituoni hapo kushiriki katika
shughuri za kijamii lakini kwa misaada yao na zawadi walizowabebea watoto
wenzao nifaraja kubwa kwa wauguzi wao na wagonjwa kwa ujumla.
Aidha
Dkt.Mwambasanga aliwataka wadau na viongozi wa shule mbalimbali wilayani hapa
kuiga mfano wa kituo hicho ambacho kinatambua umuhimu wa kuwatembelea wagonjwa
kwani kwa kufanya hivyo wagonjwa watafarijika kutokana na hali halisi kuwa
shule za wilaya ya Ludewa hazina utamaduni wa kuwatembelea wagonjwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment