Kulia meneja wa Bank ya NJOCOBA Ludewa Bw.Felix Kapinga akiwa na Meneja uwezeshaji wa Bank ya wananchi Njombe(NJOCOBA) Bw.Danford Mfikwa wakiwaelekeza wananchi namna ya kufifadhi fedha kwa njia ya Vibubu
Kulia meneja wa Bank ya NJOCOBA Ludewa Bw.Felix Kapinga akiwa na Meneja uwezeshaji wa Bank ya wananchi Njombe(NJOCOBA) Bw.Danford Mfikwa wakiwaelekeza wananchi namna ya kufifadhi fedha kwa njia ya Vibubu
wananchi wa kijiji cha Kimelembe wakifuatilia mafunzo hayo
Wananchi wa kitongoji cha Idusi kata ya Nkpmang'ombe wakifuatilia mafunzo kutoka NJOCOBA
Meneja uwezeshaji wa Bank ya wananchi Njombe(NJOCOBA) Bw.Danford Mfikwa
akitoa elimu ya uwekaji wa fedha katika bank hiyo kwa wananchi wa
kitongoji cha Idusi kata ya Nkomang"ombe
Wananchi
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wametakiwa kuacha mazoea ya kuhifadhi
fedha majumbani na badala yake wawe na utaratibu wa kufungua account katika
mabenki ili kuhakikisha fedha zao zipo katika mikono salama hasa kipindi hiki
ambacho Serikali inatarajia kuwalipa fidia wananchi wanaoishi karibu na maeneo
ya machimbo ya chuma na makaa yam awe.
Hayo
yamezungumzwa jana katika kijiji cha Kimelembe kata ya Nkomang’ombe wilayani
hapa na Mkurugenzi mtendaji wa benki ya wananchi Njombe(NJOCOBA) Bw. Michael
Nkwira katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ukiwa na lengo la
kuwaandaa wananchi kuzitumia fedha hizo za fidia ya maeneo yao katika maumizi
sahihi.
Bw.Ngwira
alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wananchi wa hilaya ya Ludewa hasa kata ya
Mundindi na Nkomang’ombe kuwa na utaratibu wa kuhifadhi fedha zao benk kwani
tabia ya kuhifadhi fedha majumbani kw kuziweka katika mabegi au kuzifukia chini
ni hatari kwani hedha hizo huibiwa au kuharibiwa na unyevu pamoja na Panya.
Alisema
Serikali inatarajia kuwalipa zaidi ya shilingi bilioni kumi kama fidia kwa wananchi
wa maeneo ya mradi ili kupisha maeneo hayo ya Chuma na Mkaa wa Mawe kwa
wawekazaji hivyo ni vyema wananchi wakaanza kufungua account katika bank ya
wananchi Njombe(NJOCOBA) ili waweze kuzihifadhi fedha zao kutokana na benk hiyo
kutokuwa na makato ya kila mwezi.
“Tunawaelimisha
wananchi jambo la uhifadhi wa fedha kutokana na ukweli kwamba wanamazoea ya
kuhifadhi fedha majumbani kwani mtu unaweza ukamkuta anazaidi ya milioni kumi
ndani ya nyumba lakini hana mpango wa kuziweka benk,jambo hilo ni hatari kwake
maana hata wezi wanaweza kumvamia na wakazichukua hivyo wanatakiwa kuziweka
katika benk yao ya wananchi ambapo ni katika mikono salama”,alisema Bw.Nkwira.
Meneja
uwezeshaji wa bank ya wananchi Njombe(NJOCOBA) Bw.Danford Mfikwa alisema kuwa
licha ya kujifunza kuweka fedha zao katika Benk pia wanatakiwa kupanga matumizi
sahihi ya fedha hizo ambazo watalipwa na Serikali kwani wengi wao huzitumia
fedha hizo kwa starehe lakini mwisho wa siku huanza kuilaumu Serikali baada ya
kuwa na maisha magumu.
Bw.Mfikwa
alisema ni vyema kila mmjoa akawa anatambua na kuwa na mipango mizuri ya
matumizi wa fedha na kama mtu atakuwa hajafikiria fedha hizo azifanyie nini ni
bora akazihifadhi katika bank ya wananchi Njombe ili kutuliza akili kwani walio
wengi hawajawahi kushika fedha nyingi kwa wakati mmoja hali ambayo itasababisha
matumizi mabaya ya fedha pamoja na kuibiwa wasipokuwa makini.
Aidha
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Diwani wa kata ya
Ibumi Mh.Edward Haule uliushukuru uongozi wa Benki ya wananchi Njombe(NJOCOBA)
kwa kukumbuka kutoa elimu hiyo mapema ili mwisho wa siku kupunguza lamawa ya
nini kifanyike baada ya mgao wa fedha hizo za fidia kwa wananchi.
Mh.Haule
alisema kuwa mpaka sasa kumekuwa na maswali mengi kutoka kwa wananchi ni lini
fidia hiyo italipwa kwani wananchi wanashindwa kufanya maendeleo katika maeneo
yao ili kupisha mradi huo na hawana fedha za kuwawezesha kuanza kujiahamisha
hivyo Serikali inapaswa kufanya mchakato huo haraka kama taarifa ilivyotolewa
Bungeni.
MH.Haule aliwataka
wananchi kutumia fulsa hiyo ya elimu waliyoipata kutoka kwa uongozi wa Benki ya
Njocoba ili kwenda na wakati kwani nyakati za kuhifadhi fedha majumbani ni
kujitafutia matatizo kwa majambazi pia mtu anaweza akafariki ghafla na familia
isijue mzazi wao alikuwa akiweka wapi na kuiacha familia katika maisha magumu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment