watoto waliotoka kijiji cha Nindi wakiwa tayari wameshapokelewa na uongozi wa Nicopolis Academy
uongozi wa Nicopolis Academy wakiwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Nindi pamoja na viongozi wa Umoja Nindi group
Mkurugenzi wa Nicopoli akiwa na meneja wa Nicopolis Academye
viongozi wa Uomja Nindi group wakiwa katika kicha ya pamoja
Mwenyekiti wa kijiji cha Nindi Bi.Zitha Haule
Kituo cha
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kijulikanocho kwa jina la NICOPOLIS
Academy kilichopo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kimeanza kuwapokea
watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutoka vijiji vya wilaya ya Ludewa kwa
lengo la kuwapa matunzo mazuri pamoja na elimu.
Akiwapokea
watoto kumi wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka kijiji cha Nindi kata
ya Lupingu wilayani hapa jana Mkurugenzi wa kituo hicho Bw.Augustino Mwinuka
alisema kuwa mpango huo wa kuwapokea watoto hao ni endelevu kutokana na lengo
la uanzishwaji wa kituo hicho licha ya kuwa ukata wa fedha ni mkubwa lakini
watapokelewa kwa awamu.
Bw.Mwinuka alisema
kuwa watoto hao wa kutoka kijiji cha Nindi wametambuliwa na kikundi cha ujamaa
Nindi group chini ya uongozi wa kijiji ni yatima na wanaishi katika mazingira
hatarishi lakini kupitia michango ya wanachama wa NICOPOLIS Academy watasaidiwa
kuishi kituoni hapo ambapo wataweza kupata elimu itakayowasaidia katika maisha
yao.
Alisema
richa ya kuwa kituo hicho kinachukua watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi na wenye ulemavu wa Ngozi pia wapo watoto ambao wameletwa na wazazi
wao kwa lengo la kupata elimu bora inayofundishwa kituoni hapo kwa kulipia
gharama nafuu ili kukiendeleza kituo kiweze kujitegemea.
“Kata ya
Lupingu na vijiji vyake kuna watoto wengi wanaoishi mazingira magumu lakini
kutokana na uhaba wa kifedha katika kituo chetu tumeona tuwachukue watoto kumi
kwanza waanze masomo lakini kama tutapata ufadhiri tutazunguka vijiji vyote
wilayani Ludewa ili kuwakusanya walau watoto ishirini kila kijiji ambao
watanufaika na elimu tunayoitoa kwani wilaya ya Ludewa kuna idadi kubwa ya
watoto wa namna hiyo”,alisema Bw.Mwinuka.
Naye
Mwenyekiti wa kikundi ya Ujamaa Nindi Bw.Germanus Lukuwi alisema kuwa kikundi
chao kinajishughurisha na mambo mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji hivyo kwa
kushirikiana na Nicopolis academy kimeona kiwasaidie watoto hao kumi waweze
kupata elimu na malezi bora hapo.
Bw.Lukuwi
alisema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi wilayani Ludewa kutokana na wazazi wao kufariki kwa maradhi
mbalimbali lakini wahisani wa kuwasaidia watoto hao bado ni tatizo hivyo
kupitia ujamaa Nindi group wakiungana na Nicopolis Academy wameanza kuona
ukubwa wa tatizo hilo na kulifanyia kazi.
Aidha
Mwenyekiti wa kijiji cha Nindi kata ya Lupingu wilayani Ludewa Bi.Zitha Haule
alikipongeza kituo cha Nicopolis Academy kwa hatua waliyoanza nayo ya
kuwachukua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuanza kuwahudumua
katika kituo chao kwani kumekuwa na changamoto nyingi inayowakabili watoto hao.
Bi.Zitha
alisema kiwa ni vyema vituo na Mashirika yasiyo ya Kiserikali yakaiga mfano wa
Nicopolis Academy kwa kuwafikia walengwa moja kwa moja na kuwasaidia kwani kuna
baadhi ya taasisi hushindwa kupitia katika Serikali za vijiji zinapotaka kutoa
huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na baadae huacha lawama
kubwa katika Serikali za vijiji kutoka kwa wananchi kuwa kuna upendeleo wa
utambuzi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment