Shamba la miti la mzee Aidan Ngailo Wipata
Mzee Aidan Ngailo Wipata akiwa shambani kwake
Shamba la mboga
Shamba la miti
Wazee
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wametakiwa kujikita katika kilimo cha
mbogamboga na upandaji wa miti badala ya kukaa na kucheza bao pia kushida
katika vilabu vya pombe za kienyeji ili kujikwamua kiuchumi na kuacha dhana ya
utegemezi ya kusubiri misaada kutoka kwa watoto na wajukuu wao wanaoishi mijini.
Hayo
yamesemwa jana na Mzee Aidan Ngailo alimaalufu kwa jina la Wipata shambani
kwake kitongoji cha Kibito kijiji cha Madindo kata ya Ludende wilayani Ludewa
alipotembelewa na waandishi wa Habari ili kujionea mafanikio ya maze huyo
mwenye umri wa miaka 68 ambaye amekuwa maalufu kutokana na shughuri zake za
kilimo.
Mzee Wipata
alisema kuwa Idadi kubwa ya wazee wamekuwa ni watu wa kulalamika na kuwasubiri
watoto wao wawasaidie kwa kila jambo wakati uwezo wa kuanzisha kilimo cha mboga
mbaga na matunda pia upandaji wa miti wanao lakini huishia kushinda kucheza bao
na kulewa pombe za asili vilabuni,hali hiyo sio sahihi kwani kama kila mzee
ataamua kujishughurisha hata vijana wazembe wataiga mfano huo.
Alisema kuwa
awali wakatia anaanza kilimo hicho baada ya kuacha na na kilimo cha mahindi pia
kufunga hoteli yake iliyokuwa Ludewa Mjini wazee wenzie walimcheka na kumuona
kafilisika kwani aliuhama mji na kuhamia mashambani huku nyumba zake zote
akizipangisha,lakini kwa sasa anamiliki zaidi ya Hekali miatatu za miti wakati
migomba pekee kunahekali ishilini pia mboga za majani anahekali tano.
“Mboga na
miti pamoja na kilimo cha migomba nimekuwa nikivuna fedha nyingi tofauti na
nilipokuwa ninaishi Ludewa mjini,hivi sasa kwa mwaka ninauhakika wa kuingiza
zaidi ya milioni themanini hivyo sina shida katika uendeshaji wa maisha yangu
hata wazee wenzangu niliowaacha mjini muda mwingi wakivaa tai wameanza kuniomba
ushauri kwa kuona nimefanikiwa licha ya kuwa umri umekwenda”,alisema maze
Wipata.
Alisema kuwa
alipofika katika kitongoji cha kibito alianza kwa kununua ekali tisa na kunaza
kilimo cha mboga na migomba mwaka 2011 lakini mpaka sasa anamiliki zaidi ya
ekali miatatu na tayari ameshazikatia hati miliki hivyo kuifanya Ardhi hiyo
iweze kukopesheka kiurahisi tofauti na ilivyokuwa awali.
Mzee Wipata
alisema kuwa vijana na wazee wengine baada ya kuona kuwa ananufaika na kilimo
pamoja na upandaji miti wameanza kuhangaika kutafuta mashamba wakati
wameshachelewa maeneo makubwa na yenye Rutuba wajanja kama yeye wameshayawahi
na tayari yanamilikiwa kisheria hivyo amewataka wananchi wengine wanaotaka kuwa
kama yeye kuchangamkia maeneo katika vijiji vingine vyenye rotuba.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment