Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Andrea Tsere akiongea na wananchi wa kijiji cha Mbugani
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Andrea Tsere akikabidhi fedha kwa wananchi wa kijiji cha Mbugani kata ya Mavanga wilayani hapa zilizochukuliwa na mtendaji wa kijiji hicho ikiwa ni michango ya wananchi hao.

Diwani wa kata ya Mavanga Mh.Emmanuel Ngalaligwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Mbugani kata ya Mavanga.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Andrea Tsere akikabidhi fedha kwa wananchi wa kijiji cha Mbugani kata ya Mavanga wilayani hapa zilizochukuliwa na mtendaji wa kijiji hicho ikiwa ni michango ya wananchi hao.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Andrea Tsere akikabidhi fedha kwa wananchi wa kijiji cha Mbugani kata ya Mavanga wilayani hapa zilizochukuliwa na mtendaji wa kijiji hicho ikiwa ni michango ya wananchi hao.
Mkuu wa
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Andrea Tsere ameanza rasmi kuwatumbua
maofisa watendaji wa vijiji wasio wa aminifu kwa wananchi ambao wamekuwa wakikusanya
michango ya maendeleo kwa wananchi na kufanyia matumizi yao binafsi hali
inayosababisha kurudisha nyuma maendeleo vijijini.
Akitoa tamko
katika mkutano wa hadhara kijijini hapo la kumuagiza mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Ludewa jana la kumfukuza
kazi mtendaji wa kijiji cha Mbugani kata ya Mundindi wilayani hapa kwa kosa la
kutafuna fedha za wananchi Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Tsere alisema kuwa
Serikali ya awamu ya tano haihitaji watendaji wabadhirifu.
Bw.Tsere
alisema kuwa mtendaji huyo wa kijiji cha Mbugani Bw.Otmary Kayombo
alilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu kuwa alikusanya michango ya
utengenezaji wa madawati na michango mingine kiasi cha shilingi milioni nne
laki moja na elfu therathini lakini zote alizitumia kwa matumizi yake hivyo
kuwafanya wananchi kugomea kufanya maendeleo mengine ya kijiji.
Alisema
baada ya kupata habari hizo kwa Diwani wa kata aliliagiza jeshi la polisi
wilayani hapa kumkamata ofisa mtendaji huyo na kumuweka mahabusu ndio alipo
agiza hakuna kutoka humo mpaka fedha hizo zilipwe ndipo mtendaji huyo
alipozitoa fedha hizo na kumkabidhi mkuu wa wilaya ili zikabidhiwe kwa
wananchi.
“nimewaletea
fedha zenu alizoziiba mtendaji wenu naomba niwakabidhi na pia niliamuru
akamatwe na asitoke mahabusu mpaka fedha hii ipatikane na imefanyika hivyo pia
namuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kumuandikia barua ya kumfukuza kazi pia
taratibu za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa Bw.Kayombo ambaye ni bingwa wa
kutafuna fedha za wananchi”,alisema Bw.Tsere.
Aidha
Bw.Tsere aliyaagiza mabaraza ya Ardhi ya vijiji na kata wilayani hapa
yaliyoisha muda wake kuvunjwa mara moja kwani yamekuwa yakituhumiwa kwa
upokeaji wa rushwa na kuwa ni chanzo cha migogoro ya Ardhi wilayani hapa ambayo
imekuwa ikirudisha maendeleo ya wananchi nyuma.
Naye Diwani
wa kata ya Mavanga Mh.Emmanuel Ngalaligwa kupitia chama cha mapinduzi alisema
kuwa mtendaji huyo wa kijiji amekuwa ni kero kwa wananchi kutokana na ukweli
kwamba kila kijiji anachopelekwa hutolewa kwa kashfa ya ubadhirifu hivyo
alichokifanya mkuu wa wilaya ni sahihi kwani wananchi wamefurahishwa kwa
maamuzi yaliyotolewa na mkuu wa wao.
Mh.Ngalaligwa
alisema kuwa wilaya ya Ludewa ni wilaya ya Tajiri pia wananchi wake ni wapenda
maendeleo lakini hurudishwa nyuma kutokana na kuwa na watendaji wasio waaminifu
hivyo tukio hila la kukamatwa mtendaji wao na kufukuzwa kazi liwe fundisho kwa
watendaji wengine wenye tabia za namna hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment