Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

July 16, 2016

MWALIMU ABAKA WANAFUNZI 12 MIONGONI MWAO NANE AMALIZANA NA WAZAZI NJE YA MAHAKAMA.

 Huyu ndiye Mwalumu Abute Fungo wa shule ya msingi Kimelembe anayetuhumiwa kuwabaka wanafunzi wake


 Mwalimu Fungo akiwa chini ya ulinzi
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kimelembe waliojitokeza kueleza jinsi walivyobakwa na mwalimu wao




JESHI la polisi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe linamshikilia Abute Fungo 40 mwalimu shule ya msingi Kimelembe kata ya Nkomang’ombe Ludewa kwa tuhuma za kubaka wanafunzi wake na kufanya udharirishaji kwa kuwapiga picha sehemu za siri na matiti huku akiwatishia kuwachapa viboko na kumuua yeyote atakayetoa taarifa popote.

Mtuhumiwa  alitenda unyama huo kwa nyakati tofauti ambapo inasadikika kati ya octoba na disemba 2015 na januari mwaka huu,Fungo alikuwa akitenda hayo polini maeneo ya kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania katika kijiji cha Kimelembe Kata ya Mkomang’ombe.

Wakizungumza na mwandishi wetu watoto wanne walioamua kutoa ushuhuda wao kabla na baada ya kufika polisi walisema mwalimu amekuwa akitenda unyama kwa  wanafunzi kila mwaka na kuongeza kuwa wenzao zaidi ya nane walishabakwa kwa kipindi cha mwaka jana na wazazi wachache kulipana nje ya mahakama.

“mimi mwalimu amenifanyia kitenda hicho zaidi ya mara nane na alikuwa akinilazimisha kumeza dawa za majira akiniambia kuwa zinazuia mimba hata hivyo nilikuwa nameza bila kutumia maji”.alisema mtoto mmoja jina tunalo

Watoto hao wenye umri chini ya miaka 14 waliongeza kuwa mwalimu alikuwa akiwalipa pesa kati ya sh500 hadi 1000 kama malipo kabla na baada ya kufanya kitendo hicho polini.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Pudenciana Protas amekiri kukamatwa kwa mwalimu huyo na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa. 

Watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kimelembe wilayani hapa walisema kuwa ubakazi huo umefanya kwa muda mrefu na mwalimu huyo lakini wamekuwa wakishindwa kutoa taarifa kwa wazazi wao na walimu wengine kutokana na kuogopa vitisho kutoka kwa mwalimu huyo.

Walisema kuwa mwalimu huyo amekuwa akitoa adhabu kali kwa mwanafunzi anayekataa kufanya naye tendo hilo hiyo imekuwa inawapa wakati mgumu wanafunzi kukataa kufanya hivyo wakihofia kuzalilishwa kwa adhabu kali mbele ya wanafunzi wengine.

Wanafunzi hao walisema kuwa walianza kuitoa siri hiyo kwa mama yao mdogo wakati wakifua nguo za shule katika mto nchuchuma ndipo mama yao mdogo huyo alipoamua kuwaeleza wazazi wao na kuchukua uamuzi wa kulipeleka jambo hilo katika Serikali ya Kijiji.

Walisema baada ya uongozi wa kijiji kupata taarifa hiyo ndipo wakaamua kutoa taarifa katika jeshi la Polisi ambapo jeshi la polisi liliamuru kukamatwa kwa mwalimu huyo na kufikishwa Mahakamani.

Wanafunzi hao wamewataka wazazi kuwa jirani na watoto wao kwani vitendo hivyo vipo na kutokana na wazazi kuwa mbali na familia zao watoto walio wengi hushindwa kuongea na wazazi wao ili kuwaeleza unyanyasaji wanaokumbana nao wakiwapo mashuleni.

Mwisho.

No comments: