Mkurugenzi mtendaji wa NICOPOLIS ACADEMY Bw.Augustino Mwinuka akisoma ripoti ya kituo hicho na changamoto zake
viwanja vya watoto vya kituo cha NICOPOLIS ACADEMY
Raia wa Ujerumani wakiwa na wenyeji wao katika kituo cha NICOPOLIS ACADEMY
PROF; LUDWIG GERNHARDT raia wa ujerumani akiwatambulisha alioongozana nao na kueleza dhumuni la msaada wake
Watoto wenye ulemavu wa Ngozi wanaotunzwa katika kituo hicho
Mwenyeji wa Wajerumani hao Bw.Willybad Mwinuka akiwakaribisha wageni wake
PROF; LUDWIG GERNHARDT akitoa zawadi kwa watoto hao
Ngoma ya saili ya Mganda kutoka Boma la Mzalendo ikitumbuiza katika ugeni huo
Mkurugenzi wa kituo hicho na wageni wake wakifuatilia burudani kutoka katika vikundi vya ngoma
Kituo cha
watoto waishio katika mazingira hatarishi na wenye ulemavu wa ngozi
kijulikanacho kwa jina la NICOPOLIS ACADEMY PRE and PRIMARY ENGLISH MEDIUM
SCHOOL kilichoko wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ambacho kinakabiliwa na
changamoto kubwa ya fedha ya uendeshaji wa kituo hicho hivi karibuni kiliweza
kutembelea na raia wa Ujeruman na kujua changamoto zao.
Akiwakaribisha
wageni hao kutoka nchini Ujeruman ambao ni familia ya Mkurugenzi PROF; LUDWIG GERNHARDT mtendaji wa
kituo hicho Bw.Augustino Mwinuka alisema kuwa kituo hicho ambacho kinaonesha
kuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Ludewa kwa siku za mbeleni kimekuwa
kikiendeshwa kwa michango ya wafadhiri wan je ya nchi na ndani japokuwa ni
kidogo lakini hakuna namna.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa PROF; LUDWIG GERNHARDT amekuwa msaada mkubwa kwani mpaka sasa kuna
baadhi ya vitu ambavyo ameshakisaidia kituo hicho kama vile vitanda kumi double
deck na magodoro yake,vitanda viwili vya watumishi na magodoro yake,meza mbili
na viti vitano vya ofisini,viti ishirini vya wanafunzi.
Vifaa
vingine ni blanket ishirini na mashuka ishirini ya wanafunzi komputa moja na
modem moja,vitabu vyenye thamani ya shilingi laki mbili,kuku jogoo mmoja,mbuzi
mmoja,mayai arobaini na nane na lita tano za Asali hivyo kukifanya kituo hicho
kupata ahueni ya namna ya kujiendesha.
“Kituo chetu
ni kichanga lakini ni msaada mkubwa kwa wanaludewa kwani mpaka sasa limeshakuwa
kimbilio la wengi ingawa bado tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa
fedha za kununulia mahitaji kwaajili ya watoto hawa hivyo tunaiomba jamii
kutuunga mkono kwani ni kituo pekee wilayani Ludewa kinachoendeshwa na watu
binafsi na kwa michango ya wadau”,alisema Bw.Mwinuka.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa uongozi wa kituo hicho umeamua kuanza ufyatuaji wa tofari kwaajili
ya kujengea mabweni ya wanafunzi ndani ya mwaka huu kwani kituo kinatarajia
kupokea wanafunzi zaidi ya 200 baada ya miaka miwili kwani uhitaji wa watoto
kuomba nafasi katika kituo hicho ni mkubwa lakini wameshindwa kuwapokeakutokana
na ukweli kwamba hakuna vyumba vya kuwalaza.
Mkurugenzi
wa kituo hicho anawaomba wananchi na wadau mbalimbali kuchangia kwa hali na mali
ili kuweza kukamilisha ujenzi wa mabweni hayo kwani watoto hao mpaka sasa
wanaishi katika nyumba ya mtu ambako kituo kimelazimika kuikodi na kuiweka kama
bweni la watoto hao.
Akiongea na
wananchi pamoja na uongozi wa kituo hicho hivi karibuni alisema kuwa PROF;
LUDWIG GERNHARDT baada ya kuombwa msaada
wa kuchangia kituo cha NICOPOLIS ACADEMY
aliguswa na changamoto wanazokabiliana nazo hivyo yeye na familia yake waliona
ni vyema wakajitolea msaada huo.
PROF; LUDWIG
GERNHARDT alisema kuwa imekuwa kawaida yeye kutoa misaada mbalimbali katika
nchi ya Tanzania hasa wilaya ya Ludewa katika vikundi na shule mbalimbali
lakini mara nyingine anavunjika moyo pale anapoona misaada hiyo haitumiki kama
ilivyoombwa na walengwa.
Aliwaasa
viongozi wa kituo hicho kutoshawishika na wengine wenye nia ovu na misaada ya
wafadhiri badala yake waendelee kuwaomba wadau mbalimbali katika kuhakikisha
watoto hawa wenye mazingira hatarishi na wenye ulemavu wa ngozi wanapata maisha
bora hivyo ataendelea kuunga mkono juhudi hizo ambazo zimeanza vizuri na
zinaonekana kwa macho.
Aidha
mwenyeji wa Wajerumani hao nchini Tanzania ambaye ndiye alikuwa akiwatembeza
maeneo mbalimba nchi Bw.Willbad Mwinuka alisema kuwa ugeni huo umekuwa ni ugeni
wa Baraka kubwa wilayani Ludewa kwani ni miaka mingi hivi sasa wamekuwa wakitoa
misaada mbalimbali hasa katika kuwalipia ada za shule watoto wanaoishi
mazingira hatarishi.
Bw.Mwinuka
alitoa angalisho kuwa wale wote wanaopata misaada na vitu mbalimbali kutoka kwa
Mjerumani huyo wanapaswa kufikishwa kwa walengwa kama vilivyo ili kumtia moyo
mfadhiri kuendelea kuifadhiri wilaya ya Ludewa pia jamii inayoguswa na uwepo wa
watoto hao inapaswa kujitolea na sio kusubiri kutoka kwa wenzetu wan je ya nchi
kwani iko siku moja watasitisha kutusaidia.
Mwisho.
Mkurugenzi wa
kituo sim no 0765059184
No comments:
Post a Comment