Bw.Ocol Haule akitoa ufafanuzi kuhusiana na mradi huo wa ufugaji wa samaki katika mabwawa ambayo tayari yamekamilika ikiwa bado kuingiza maji na kuanza rasmi ufugaji wa samaki
Bw.Ocol Haule akitoa ufafanuzi kuhusiana na mradi huo wa ufugaji wa samaki katika mabwawa ambayo tayari yamekamilika ikiwa bado kuingiza maji na kuanza rasmi ufugaji wa samaki
Mabwawa ya Samaki ambayo yako dayari na kubakia kazi moja ya uingizaji wa maji na Vifaranga wa Samaki
Mabwawa ya Samaki ambayo yako dayari na kubakia kazi moja ya uingizaji wa maji na Vifaranga wa Samaki
vijana wakiendelea na kazi ya uchimbaji wa mabwawa ya samaki katika mradi huo mkubwa aliouanzisha bwana Ocol Haule

Vijana wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wametakiwa kujikita katika uwekezaji usio na gharama kubwa ambao ni ufugaji wa Samaki ili kujikwamua kiuchumi kwa wamekuwa wakijikita katika miradi mingi ambayo uendeshaji wake huhitaji gharama kubwa hali inayowafanya washinde kuiendesha miradi na kubaki katika wimbi la umaskini.
Hayo yamesemwa leo na mmoja wa vijana wilayani hapa Bw.Ocol Haule ambaye ameamua kujikita katika uwekezaji mkubwa wa samaki kwa kichimba mabwawa ya awali 11 akiwa na lengo la kufanya ufugaji huo ambao lengo kubwa ni kujipatia kipato na kugawa vifaranga wa samaki hao katika vikundi vya wafugaji ambavyo vitakuwa tayari kufanya ufugaji.
Bw.Haule alisema kuwa jamii ya Ludewa bado haina mwamko wa kubuni miradi kama ufugaji wa samaki ambayo inaweza kuwa ni chanzo kimajawapo cha kipato miongoni mwa jamii licha ya kuwa wilaya ya Ludewa inafulsa nyingi za uwekezaji kikiwemo kilimo na ufugaji lakini bado elimu kwa wananchi kuhusu kuzitumia fulsa hizo haijapita kikamilifu.
Alisema kuwa uanzishwaji wa mradi huo wa ufugaji wa samaki ni fulsa tosha kwa wananchi wa maeneo ya Ludewa kijijini ambako mabwawa hayo yanachimbwa kuanza kuchimba mabwawa yao kwa kila mwananchi ili kuweza kufuga taratibu kutokana na uwezekano mkubwa wa upatikanaji mbegu za samaki kutoka katika mabwawa yake.
"Wengi wamekuwa wakinishangaa kwa hili ninalolifanya ,lakini ukweli usiopingika mpango huu ni mpango endelevu ambao mwisho wa siku utaleta tija kwa wilaya kwani nimejifunza kutoka kwa Padre Merodious Mlowe kule kata ya Mundindi alianza kama utani lakini kwa sasa yuko mbali katika uzalishaji wa samaki na matunda,hivyo nawasihi wananchi hasa vijana kufanya ufugaji wa samaki katika vikundi na vifaranga wa mbegu nitatoa bure kwa watakao hitaji kufanya ufugaji",alisema Bw.Ocol Haule.
Alisema kuwa uanzishwaji wa mradi huo wa ufugaji wa Samaki umewahusisha wataalamu mbalimbali wanaojua kanuni na taratibu za uchimbaji mabwawa na ufugaji wa samakia kwani bila kufanya hivyo inakuwa shida katika kujua nini samaki anahitaji na muda gani samaki anatakiwa kuvuliwa.
Bw.Haule alisema kuwa lengo kubwa ni kuchimba mabwawa zaidi ya miamoja ambayo yatakuwa na samaki waliofugwa vizuri na kwa ubora ili wafikapo wawekezaji wa miradi ya Chuma cha Liganga na Makaa ya mawe ya Nchuchuma wasiende kutafuta samaki wa kitoweo katika wilaya nyingine zaidi ya hapa wilayani Ludewa.
Kuhusu gharama za uchimbaji wa mabwawa na ufugaji wa samaki hao Bw.Haule alisema kuwa hakuna gharama kubwa kwani samaki ni mnyama au kiumbe anayekula kiasi kidogo sana cha chakula tofauti na viumbe wengine wanaofugwa Duniani pia gharama za uchimbaji wa bwawa moja ni makubaliano tu na wachimbaji haizidi shilingi laki moja na hiyo ni kutokana na ukubwa wa bwawa.
Aidha mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Ludewa kijijini ambako mradi huo mkubwa wa bwana Ocol Haule wa ufugaji wa Samaki unatekelezwa Bw.Silivesta Mdanga alisema kuwa mradi huo ni fulsa kubwa kwa wananchi wa kijiji chake kwani awali walitamani kufuga samaki lakini walikosa mahali pa kuwata vifaranga wa samaki.
Bw.Mdanga alisema kuwa kupitia mabwawa hayo ambayo yatazalisha aina mbalimbali za samaki vijana wengi wataweza kufanya ufugaji kutonana upatikanaji wa vifaranga wasio na masharti ambapo sharti lao ni kuunda vikundi vya ufugaji samaki na kwenda kuchukua vifaranga bure na kuanza ufugaji usio na gharama.
Bw.Mdanga aliwataka wananchi wa kijiji chake kuchangamkia fulsa hiyo ili kuweza kuboresha maisha ya kila mwananchi mmoja mmoja kwani kwa kufanya ufugaji huo wa samaki ambao tayari neema imeangukia katika kijiji chake maisha ya wananchi wake yatabadirika na kuwa na maisha mapya yenye uchumi mzuri tofauti na maisha ya asawali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment