Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 24, 2016

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yateua Wabunge Watatu wa Viti Maalumu.....Taarifa Kamili Iko Hapa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewateua ndugu Ritha Enespher Kabati na ndugu Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndugu 
Lucy Fidelis Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa Wabunge Wanawake wa viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa Tume katika Kikao chake cha tarehe 11/11/2015 ilifanya Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum 113 kwa mwaka 2015. Hata hivyo, Wabunge Wanawake wa Viti Maalum walioteuliwa jumla yake ilikuwa ni 110 kati ya 113 ambapo Viti vitatu (3) vilibakizwa kusubiri Uchaguzi wa Majimbo nane (8) ambayo Uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali.
Uteuzi wa awali ulihusisha Vyama vitatu vilivyofikisha asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Wabunge kama matakwa ya Katiba yanavyotaka.  Vyama vilivyopata asilimia tano ambayo ilikuwa 780,226 ni.
Na.
Jina la Chama
Idadi ya Kura baada ya majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge
1.
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
8,332,953
2.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
4,627,923
3.
Chama cha Wananchi (CUF)
1,257,051

Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Majimbo hayo nane (8), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ndivyo vilivyoendelea kupata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge, kwa maana hiyo, vyama hivyo ndivyo vitaendelea kuhusishwa kwenye Mchakato wa kugawanywa hivyo Viti 3 vilivyobaki.

IDADI YA KURA ZA CCM, CHADEMA NA CUF BAADA YA UCHAGUZI WA MAJIMBO NANE (8) KUKAMILIKA
Baada ya kukamilika Uchaguzi katika majimbo nane (8) Idadi ya Kura kwa Vyama vya CCM, CHADEMA na CUF ni kama ifuatavyo:

Na.
Jina la Chama
Idadi ya Kura baada ya majimbo 256 kufanya Uchaguzi wa Wabunge
Idadi ya Kura baada ya Uchaguzi wa Majimbo nane (8) kukamilika
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge.
1.
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
8,332,953
162,535
8,495,488
2.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
4,627,923
92,958
4,720, 881
3.
Chama cha Wananchi (CUF)
1,257,051
17,860
1,274,911
                                                                                                               
1.0.  MGAWANYO WA VITI VITATU (3) VYA WABUNGE WA VITI MAALUM
Kukamilika kwa Uchaguzi wa majimbo nane (8) kumeonesha kuwa, Viti vitatu vilivyosalia vitagawanywa kwenye vyama viwili vya CCM na CHADEMA kwa mpangilio ufuatao:
CHAM A CHA MAPINDUZI (CCM)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Mapinduzi ni 8,495,488. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CCM:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CCM kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
8,495,488  X 113
= 66.24 ambayo ni 66
14,491,280


Hivyo, CCM watakuwa na Viti 66 vya Wabunge wa Viti Maalum, awali walikuwa na viti 64.

CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CUF kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
1,274,911 X 113
= 9.9 ambayo ni 10
14,491,280


Hivyo, CUF wataendelea kubakia na Viti 10 kwa kuwa katika Chaguzi za Majimbo nane (8) hawakuweza kuongeza Kura ambazo zingewaongezea Idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni 4,720, 881. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CHADEMA:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CHADEMA kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
4,720,881  X 113
= 36.81 ambayo ni 37

14,491,280


Hivyo, CHADEMA watakuwa na Viti 37 vya Wabunge wa Viti Maalum, awali walikuwa na viti 36.

CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ilizopata Chama Cha Wananchi (CUF) ni 1,274,911. Hivyo ili kujua Idadi ya Viti Maalum kitakachopata CUF:
Jumla ya Kura zote halali za Ubunge ambazo CUF kimepata unazidisha kwa Idadi ya Viti Maalum vyote na kugawanya kwa Idadi ya Kura halali za Ubunge kwa vyama vilivyopata angalau asilimia tano ya Kura zote Halali za Ubunge. Hivyo,
1,274,911 X 113
= 9.9 ambayo ni 10
14,491,280


Hivyo, CUF wataendelea kubakia na Viti 10 kwa kuwa katika Chaguzi za Majimbo nane (8) hawakuweza kuongeza Kura ambazo zingewaongezea Idadi ya Wabunge wa Viti Maalum.

MAPENDEKEZO YA MAJINA YA UTEUZI WA VITI MAALUM KWA VYAMA VYA CCM NA CHADEMA
Tume hufanya uteuzi kwa kufuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na Katibu wa Chama husika, kwa mantiki hiyo Tume imewateua Wabunge hao kama ilivyojitokeza katika orodha za Vyama vya CCM na CHADEMA.
 Katika orodha iliyowasilishwa na CCM majina nambari 65 naa 66 ni
65.  Ndugu Ritha Enespher Kabati
66.Ndugu Oliver Daniel Semuguruka.
Katika Orodha iliyowasilishwa na CHADEMA jina nambari 37 ni
37. Ndugu Lucy Fidelis Owenya.
Asanteni  kwa kunisikiliza,

Jaji Mst Mh. Damian Z. Lubuva
MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

No comments: