Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

April 14, 2016

SHULE ZISIZOTOA HUDUMA YA CHAKULA SHULENI MARUFUKU KUWAPA WANAFUNZI DAWA ZA KICHOCHO

 Wanahabari na maofisa Habari wa Mkoa wa Njombe wakishiriki semina ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele Mjini Njombe





 Baadhi ya Washiriki wanahabari Toka Mkoa wa Njombe Wakiwemo Maafisa Habari wakiwa kwenye semina ya Magonjwa yasiyopewa kipaumbele


Wanahabari Toka Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe Wakishiriki Semina ya Magonjwa yasiyopewa kipaumbele iliyoandaliwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii Wazee na Watoto Mjini Njombe Muda Huu.



Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia Wazee na Watoto Imepiga marufuku walimu kuwapa wanafunzi dawa za kichocho kama huduma ya chakula shuleni haitolewi.

Kauli hiyo imetolewa na  Mratibu wa mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Upendo John Mwingira   Toka Wizara ya Afya katika semina iliyowakutanisha wanahabari na Maofisa Habari wa Mkoa wa Njombe ikilenga kuwaelimisha wanahabari namna ya kwenda kutoa elimu sahihi juu ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele ukiwemo ugonjwa wa Kichocho.

Bi.Mwingira Amesema Pamoja na kuwepo na magonjwa 17 yasiyopewa kipaumbele duniani lakini ugonjwa wa kichocho umeonekana dawa zake kuleta madhara kwa watumiaji endapo watakunywa bila kula chakula hususani kwa shule ambazo hazitoi chakula cha mchana.

Aidha ameeleza kuwa wanahabari wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya magonjwa hayo baada ya serikali kuliona tatizo la magonjwa yasiyopewa kipaumbele na kulipa uzito kwa kuanza kutoa kingatiba.

Katika Hatua Nyingine Amewataka Wanahabari kutambua kuwa magonjwa hayo kama Kichocho,Mabusha,Matende,Trakoma pamoja na Minyoo ni ugonjwa ambao endapo usipopewa uzito unaweza kuleta madhara makubwa vikiwemo vifo.

Amesema takwimu zinaonesha kuwa watu milioni 200 duniani kote wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa 
kichocho huku watu milioni 20 wameshaathirika na ugonjwa huo.

Akizungumzia ugonjwa wa Minyoo amesema takribani watu bilioni 2 wameathirika na ugonjwa huo huku watu 155 wakiripotiwa kufa  kutokana na minyoo.

Kwa upande wao wanahabari Kutoka vyombo mbalimbali vya habari walioshiriki semina hiyo wameahidi kwenda kutoa ushirikiano wa kutosha katika kutoa elimu stahiki juu ya magonjwa hayo huku wakiwataka wananchi kutoa ushirikiano pindi zoezi hilo linapofanyika katika maeneo yao.

Hata Hivyo wamewataka wataalamu wa Afya kuwashirikisha kwa kila hatua ya udhibiti wa magonjwa hayo ili kwenda sawa pindi jamii inaposhindwa kufahamu baadhi ya Mambo.

No comments: