Dr. Shein Aapishwa Rasmi Kuwa Rais wa awamu ya 7 wa Zanzibar
Rais
Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
ameapa kuwa Rais kwa mujibu wa katiba katika kuongoza wananchi wa
Zanzibar kwa muda wa miaka 5.
Rais
Mteule ameapishwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omary Othman Makungu
mbele ya viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa dini na kushuhudiwa na
mamia ya wananchi katika uwanja wa Amani mjini Unguja.
Baada
ya Rais Shein kuapishwa viongozi wa dini wameomba dua wakiongozwa na
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis na kufuatiwa na Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Mhashamu Augustino Shayo na
Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh.
Viongozi
mbalimbali wamehudhuria Kiapo hicho akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, viongozi wastaafu wa kitaifa na mamia ya
wananchi.
Aidha
Rais Dkt. Ali Mohamed Shein ameapishwa na kuwa Rais wa awamu ya saba
kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na kukagua gwaride rasmi, pamoja
na itifaki nyingine kufuatia.
No comments:
Post a Comment