Miti inayohifadhi maji ikiwa imepandwa
kaimu meneja wa mamlaka ya maji Ludewa Bw.Gregory Mwinuka akipanda miti katika chanzo kimojawapo cha maji Mapetu siku ya kilele cha wiki ya maji
Bw.Esau Haule ni mmoja wa wananchi waliokubali kuachia maeneo yao ili kuhifadhi vyanzo vya maji
kazi ya upandji miti ikiwa inarndelea
Kilele cha
wiki ya maji wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kimeadhimishwa kwa upandaji
miti katika vyanzo vya maji katika maeneo ya Mapetu huku wananchi wakikubali
kuachia maeneo yao ambayo yako katika vyanzo hivyo awali yalitumika kama mashamba
yao ili kuweza kupata maji kwa wingi katika uhifadhi wa Vyanzo hivyo.
Akiongea na
waandishi wa habari mmoja wa wananchi wenye maeneo katika vyanzo hivyo ambaye
alishiriki katika upataji wa miti inayoweza kuhifadhi maji Bw.Esau Haule
alisema kuwa awali vyanzo hivyo vilitumika kama mashamba ya vinyungu na kuweza
kuwasaidia wakulima hao katika kipato lakini walipotakiwa kuayaachia maeneo
hayo walifanya hivyo bila kukaidi.
Bw.Haule
alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa hakuna asiyejua umuhimi wa maji katika
matumizi ya binadamu hivyo tamko la Serikali la kupisha eneo hilo la Mapetu ili
kuweza kuhifadhi chanzo hicho cha maji hakuna mwananchi ambaye alipinga na
hivyo yeye ambaye alikuwa na eneo kubwa katika chanzo hicho amelazimika
kushiriki kikamilifu kupanda miti ambayo itaendeleza utunzaji wa chanzo hicho.
Alisema kuwa
kuna baadhi ya wakulima bado hawanaelimu ya kutosha kuhisiana na kuhifadhi
vyanzo vya maji hivyo Serikali inapaswa kutoa elimu mara kwa mara kwani
asilimia kubwa ya wakulima wa wilaya ya Ludewa bado wanatabia ya kulima katika
vyanzo vya maji hasa nyakati za kiangazi.
Bw.Haule
alisema changamoto kubwa inayovikabili vyanzo vya maji ni pamoja na uchomaji
moto kwa wawindaji na wachomaji mkaa ambapo moto hutoroka na kuteketeza magugu
yanayosaidia utunzaji wa vyanzo hivyo hali hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara
hasa baada ya msimu wa mvua kuisha hivyo Serikali inatakiwa kuwachukulia hatua
za kisheria wenye tabia hizo.
“Nimeshiriki
katika zoezi hili la upandaji miti siku ya kilele cha maji ili kuwaonesha
wananchi wenzangu umuhimu wa jambo hili kwani bila kufanya hivi wananchi
wangeweza kuona bado ninakinyogo na kutoa eneo langu ili litumike kama eneo la
kuhifadhi chanzo hiki cha maji,hivyo nawaomba wengine kuiga mafano huu”,alisema
Bw.Haule.
Naye kaimu
meneja wa mamlaka ya maji Ludewa Mjini Bw.Gregory Mwinuka alisema kuwa mpango
wa Serikali ni kuhifadhi vyanzo vyote vya maji wilayani Ludewa ili kuweza kutoa
huduma ya maji safi na salama kwa wananchi isiyo na mashaka msimu mzima wa
mwaka.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa ifikie wakati wananchi watii sheria bila shuruti kwa kuacha
kuvamia vyanzo vya maji na kulima mazao ya chakula nay ale ya kibiashara kwani
kwa kuvitunza vyanzo hivyo kero ya uhaba wa maji itatoweka na kuwafanya
wananchi wakifanya shughuri nyingine za kimaendeleo nadala ya kutafuta maji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment