KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA NJOMBE CHARLES NAKEMBETWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKWE LEO
Kamanda Nakembetwa Amesema Ubadhilifu huo Umefanyika Katika Maeneo Ya Miradi Ya Nyumba Za Walimu,Zahanati,Ofisi Za Vijiji, Miradi Ya Maji, Mishahara Hewa Kwa Watumishi Wa Halmashauri, Fedha Ambazo Zilipelekwa Na Serikali Kuu Kwaajili Ya Kutekeleza Miradi Zilikuwa Hazifikishwi Sehemu Husika Ambayo Serikali Ilitegemea.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU Mkoani Njombe Imesema Katika Kipindi cha Mwaka 2015 Hadi Januari 2016 Imefanikiwa Kuokoa Zaidi ya Shilingi Milioni 120 Zilizokuwa Zikitolewa Kwa Ajili ya Utekelezaji wa Miradi na Malipo Hewa Kwa Halmashauri na Vijiji Vya Mkoa wa Njombe.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkao wa Njombe Charles Nakembetwa Amesema Wamebaini Wizi na Matumizi Mabaya Yaliyokuwa Yanafanywa na Baadhi ya Watendaji wa Serikali Wasiowaaminifu Kikiwemo Kiasi cha Zaidi ya Shilingi Milioni 82 Kwa Ajili ya Kuwalipa Mishahara Watumishi Hewa Kumi Katika Hospitali ya Ilembula.
Aidha Nakembetwa Amesema Kuwa Wamebaini Kuwepo Kwa Matumizi Mabaya ya Fedha Zinazotolewa na Serikali Katika Hospitali ya Ilembula , Huku Akiahidi Kuwachukulia Hatua Kali za Kisheria Wahusika Wote Kujibu Tuhuma Zinazowakabili.
Katika Hatua Nyingine Kamanda Huyo wa TAKUKURU Ameelezea Suala la Ufufuaji wa Maduhuri ya Serikali Katika Kata ya Ramadhan Halmashauri ya Mji wa Njombe Ambapo Kiasi cha Shilingi Milioni 11 na Laki Sita Zilitumwa Kwa Utaratibu Unaoitwa Urejeshaji wa Asilimia 20 ya Mapato Yanayokusanya Kwenye Vijiji na Kata Huku Watendaji wa Kata na Vijiji Wakitumia Kwa Matumizi Yao Binafsi.
Amesema Takukuru Mkoa Wa Njombe Ilibaini Matumizi Mabaya Ya Fedha Za Ujenzi Wa Nyumba Ya Mwalimu Na Maabala Katika Kata Ya Mahongori Makambako Shilingi Laki 8 Na Elfu Sitini Zilitolewa Kwa Kazi Hiyo Lakini Hazikutumika Kama Ilivyokusudiwa ,Huku Katika Hifadhi Ya Mpanga Kipengele Kukidaiwa Kulikuwa Na Matumizi Mabaya Ya Fedha Za Ujenzi Wa Ofisi Katika Hifadhi Hiyo .
Sanjari Na Hayo Kamanda Nakembetwa Amesema Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Ilikuwa Ikilipa Mishahara Hewa Kwa Watumishi Katika Kipindi Hicho Ambapo Jumla Ya Shilingi Milioni 21 Laki Saba Na 21 Na Sent 50 Na Kwamba Halmashauri Hiyo Ilitumiwa Fedha Hiyo Kutoka Serikali Kuu Lakini Haikutumia Kwa Malengo Yaliokusudiwa Na Pesa Hizo Wahusika Wamekwisha Rejesha Hazina.
Takukuru Imesema Ubadhirifu Huo Umefanyika Katika Halmashauri Mbalimbali Za Mkoa Wa Njombe Ikiwemo Wanging'ombe,Makambako,Mahongore Makambako, Ludewa Na Maeneo Mengine Ikiwemo Mishahara Hewa Kwa Watumishi Kumi Wa Hospitali Ya Ilembula.
No comments:
Post a Comment