Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

February 08, 2016

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AWATAKA MADIWANI KUJADILI NA KUPIGA MARUFUKU BIASHARA YA RUMBESA YA VIAZI KAMA WALIVYOFANYA WAKAZI WA MKOA WA MBEYA






 HAPA MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA  NCHIMBI  AKIWASILI KWENYE MAADHIMISHO YA KILELE CHA KUTIMIZA MIAKA 39 YA KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI

 NGOMA YA ASILI  IKIONGOZA MSAFARA WA MKUU WA MKOA WA NJOMBE KWENYE MAADHIMISHO HAYO


 BAADA YA KUWASILI KWENYE ENEO LA MKUTANO MKUU WA MKOA HUYO ALIANZA NA KUZINDUA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KWANZA


 NI MTI WA MATUNDA AINA YA MAPARACHICHI




 WANACHAMA WAKIWA NA FRAHA SANA SIKU HIYO




Madiwani Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Waliochaguliwa Kupitia Chama Cha Mapinduzi  Wametakiwa  Kuweka Mipango Mikakati Ya Kutokomeza Biashara Ya Mazao  Mbalimbali Kwa  Mtindo Wa Lumbesa  Kwa Kujadili Kwenye Vikao Na Mikutano Ya Mabaraza Ya Madiwani   Ikiwemo Zao La Viazi.

Rai Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Wakati  Akiwa Mgeni Rasmi  Kwenye Kilele Cha Maadhimisho Ya  Kutimiza Miaka 39 Ya Kuzaliwa Kwa Chama Cha Mapinduzi  Ambapo  Kiwilaya Na Mkoa Wa Njombe  Yakifanyikia Katika  Mtaa Wa Itulike  Tawi La Ipui.

Aidha Dkt Nchimbi Amesema Wawakilishi Wa Kuu Wa Wananchi  Na Wanachama Wa CCM Wanatakiwa Kutambua  Uwepo Wa Majipu Katika Mkoa Wa Njombe  Ambao Ni Rumbesa Ya Viazi    Ambapo Amesema  Biashara Ya Rumbesa  Inawakandamiza Wakulima  Wa Zao La Viazi  Na Kusema Kwa Mwaka Huu Wanatakiwa Kushikamana Kuzuia Biashara Hiyo   Ili Kufanikiwa  Kama Walivyofanikiwa Wakazi Wa Mkoa Wa Mbeya Na Maeneo  Mengine.

Amesema Kuwa Chama Hicho Kinapoadhimisha Miaka 39 Ya Kuzaliwa Kwa Chama Cha Mapinduzi  Wanachama Wake Wanajivunia Kuwa Na Viongozi Wenye Uwezo Wa Kuwaongoza Na Kutatua Changamoto Za Wananchi  Hapa Nchini Huku Akiwataka Wachama  Wa CCM Kufanya  Kazi Kwa Bidii Na Uaminifu Ili Kuonesha Dira Ya Mafanikiwa Kwa  Wananchi.

Akisoma Taarifa Ya  Kuanzishwa  Kwa Chama Cha Mapinduzi   Nchini Katibu  Wa CCM Wilaya Ya Njombe Sadakatt Kimat   Amesema Chama Hicho Kilianzishwa  Na Viongozi Waasisi   Mwaka 1977   Na Hayati Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Kamparage Nyerere Na  Rais Wa Zanziba  Shekhe Abed Aman Karume  Baada Ya Kuunganisha Vyama Viwili Chama Cha TANU Na ASP  Kwa Lengo La Kuondoa Ujinga,Maradhi Na Umasikini.

Aidha Kimatt Amesema Chama Cha  Mapinduzi Kimefanya Kazi Kubwa Ya Kuhakikisha  Kinashinda Kwa  Zaidi  Ya Asilimia 70  Kwa Ngazi Ya Urais Na Asilimia  75 Kwa Ngazi Ya Udiwani Na Asilimia 72 Kwa Ngazi Ya Ubunge  Na Kwamba Chama Hicho Kitaendelea Kushika Dola  Kila Uchaguzi Huku Akiwashukuru Wanachama Kwa Kuwapatia Ridhaa Hiyo.

Katibu Mwenezi Wilaya Ya Njombe Hiltra Msola Amesema Kuna Watu Watakwenda Kuwalaghai Na Kutoa Maneno Ya Udanganyifu Kwamba Wanatakiwa Kuwa Na Mabadiliko  Lakini Hawana Uwezo Wa Kusimamia  Utekelezaji Wa Maendeleo  Na Hivyo Kuwataka Wananchi Kufanya Uchaguzi Sahihi Ili Miradi Yao Iweze Kusonga Mbele Kwa Haraka.

Katika Maadhimisho Hayo Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi  Amekabidhi Kadi Kwa Wanachama 30  Ambao Wamewakilisha Wanachama Wengine  Mia Sita Ambao Wamejiunga  Wakati Chama Hicho Kikitekeleza Majukumu Mbalimbali Ikiwemo Kutoa Misaada,Kupanda Miti Na Kufanya Usafi Kwenye Mazingira Ambapo  Hata Mkuu Wa Mkoa Kabla Ya Kuanza Kutoa Hotuba Yake Alizindua Upandaji Wa Miti Katika Tawi Hilo.

No comments: