Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 12, 2015

UJENZI WA MRADI WA UMEME KILONDO WALETA MATUMAINI

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiangalia Power House katika kijiji cha Kilondo
huu ndio mtaro wa maji kwaajili ya kufua umeme kata ya Kilondo


 Filikunjombe akipata maelezo kuhusiana na ujenzi wa mradi huo





Ujenzi wa mradi wa umeme wa kutumia maji kwa ufadhiri wa REA katika kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoa wa Njombe umeanza kuleta matumaini baada ya hatua ya awali kukamilika ambayo ni ujenzi wa njia ya maji na nyumba ya kufunga mtambo wa kufua umeme kukamilika.


Hivi karibuni mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe aliweza kutembelea mradi huo ambao uko mwambao wa ziwa Nyasa na kujionea maendeleo yake ambapo aliweza kuwashukuru wananchi kwa kushirikiana na wakandarasi wa mradi huo.


Filikunjombe alisema kuwa wakati wa utawala wake yeye kama mbunge Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kuanzisha miradi ya umeme katika vijiji 67 wakati wilaya ya Ludewa inajumla ya vijiji 77 hivyo ni vijiji 10 tu ndivyo vitakuwa havina nishati ya umeme lakini juhudi za kukamilisha miradi hiyo na kuhakikivijiji vyote vya wilaya ya Ludewa vinakuwa na nishati hiyo zinaendelea.


Aidha aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa katika vijiji hivyo 67 kushirikiana kikamirifu na wawekezaji hasa wataalamu wa miradi hiyo ili kuhakikisha miradi hiyo inakamirika haraka kwa muda uliopangwa na Serikali.


“nawaomba wananchi wa jimbo langu kushirikiana kikamirifu bila kujari itikadi za vyama vyenu kufanya kazi na wawekezaji hasa hawa wataalamu wa miradi hii ya umeme ambao wanafanya kazi ngumu katika maeneo yetu na tuondoe dhana potofu ya kuwa hizi kazi ni za Serikali wakati umeme tutautumia sisi wananchi ambao ndio Serikali yenyewe”,alisema Filikunjombe.


Naye mmoja wa wananchi wa kata hiyo Bw.George Mwakipokile alisema kuwa wananchi wamekuwa wakishirikiana kikamirifu na  mafundi wa kazi hiyo katika kila hatua kwani ni jambo la kimaendeleo kupata nishati hiyo Kilondo awali hakuna hata mtu mmoja ambaye alifikiria siku moja kata ya Kilondo ingeweza kuwa na umeme.


Bw.Mwakipokile alisema kuwa wananchi wanamshukuru mbunge wao ambye ni Filikunjombe kwa kushirikiana na Bw.Mwambeleko kubuni mradi huo wenye tija kwa jamii ya wanaludewa kwani mradi huo ni mkubwa na unauwezo wa kusambaza umeme huo katika kata zote za mwambao wa ziwa Nyasa.


Mwisho.

No comments: