Mgeni rasmi wa hafla hiyo ambaye ni ofisa kilimo wa wilaya ya Ludewa Bw.Naftari Mundo akiongea na wakulima wa kata ya Mundindi katika kijiji cha Amani
Mkulima wa kijiji cha Amani wilayani Ludewa akitoa maelekezo namna ya elimu aliyoipata na na alivyoweza kuitumia katika uzalishaji wa zao la mahindi
Afisa miradi wa shirika la ACTN Bw.Deogratias Ngotio
wakulima wakipata somo
mtaalamu wa mbegu za mahindi Bw.Mbele akiongea na wakulima
Mtaalamu wa mbolea toka YARA Bw.Shine akitoa elimu kwa wakulima
Wakulima wa
kijiji cha amani wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wamepata elimu ya kilimo
bora cha mazao ya mahindi,maharage na soya kupitia mashamba darasa ili kuweza
kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao hayo kutokana na kijiji hicho kuwa
kinara wa uzalishaji wa mazao ya aina hiyo wilayani hapa na mkoa wa Njombe kwa
ujumla.
Elimu hiyo
imetolewa hivi karibuni na wafadhiri ambao ni African conservation tillage
network(ACTN BRITEN,RUDI na CRDB BANK wakiwa na kauli mbiu isemayo “kilimo
hifadhi kwa mazao bora mavuno zaidi gharama nafuu na ardhi yenye rutuba”ikiwa
na lengo kuu la kukuza uchumi kwa wakulima ambao wataanza kufanya kazi za
kilimo kwa kisasa zaidi.
Akiongea katika
hafla ya kufunga mafunzo hayo na wakulima wa kata ya Mundindi katika kijiji cha
Amani wilayani Ludewa afisa miradi wa ACTN Bw.Deogratias Ngotio alisema
kuwa muungano wao ni kutoa mafunzo ya
miradi shirikishi ya kuongeza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini
mwa Tanzania kwa mazao ya mahindi,mpunga,maharage na soya kupitia elimu hiyo
wakulima wataweza kunafaika na kilimo.
Bw.Ngotio
alisema kuwa kilimo kimekuwa ni mzigo kwa wakulima kutokana na wakulima
kutokuwa na elimu ya kutosha ya kilimo hivyo wadau wa kilimo nchini wameona ni
bora kutoa elimu ya kilimo bora na kuhifadhi ardhi yenye rutuba ili kilimo
kiweze kuwa ni ukombozi kwa wakulima na sio mzigo wa wakulima kama inavyoonesha
katika meneo mengi.
Alisema kuwa
wakulima walio wengi wamekuwa wakilima maeneo makubwa na kupata mavuno kidogo
hali inayowakatisha tama wakulima na wengine huachana na kilimo kwa kuona hakina
faida ikiwa haya yate husababishwa na elimu duni waliyonayo wakulima wa Nyanda
za juu kusini lakini kwa kupitia wadau mbalimbali wa kilimo wanaoweza kutoa
elimu baadhi ya wakulima wameshaanda kutambua umuhimu wa kilimo katika uchumi
wa taifa na maisha yao kwa ujumla.
“tumegundua
kuwa baadhi ya wakulima wanakatishwa tama ya kuendelea na kilimo kutokana na
ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusiana na kilimo bora lakini kutokana na
muungano wetu kwa pamoja tumeweza kutoa elimu ya shamba darasa ambapo baadhi ya
wakulima wameanza kupata mafanikio kupitia mafunzo yetu hali ambayo inatupatia
moyo wa kuendelea na mafunzo haya maeneo mbalimbali ili kuweza kuwainua
wakulima katika mavuno zaidi”,alisema Bw.Ngotio.
Mmoja wa
wakulima wa Kijiji cha Amani Bw.Fransis
Mlelwa alisema kuwa kijiji hicho kinachoongoza
wilayani Ludewa na mkoa wa Njombe kwa uzalishaji wa mazao ya mahindi na
maharage ambapo mkulima wa hali ya chini anauwezo wa kuvuna magunia 1500 katika
msimu mmoja wa kilimo kwa hali hiyo mashirika mbalimbali yameweza kuungana
kuanza kutoa elimu ya kilimo bora.
Bw.Mlelwa
alisema kuwa licha ya kupata mafunzo hayo ambayo ni msaada mkubwa kwao katika
uzalishaji pia changamoto kubwa inayowakabili wakulima wa kijiji hicho ni
upatikanaji wa masoko ya mahindi wakati wa mavuno kwani kumekuwana na shida
kubwa kutokana na uzalishaji mkubwa wa mahindi walio nao.
Alisema
licha ya kuwa Serikali imekuwa ikiyanunua mahindi kupitia wakala wa hifadhi ya
chakula ya Taifa lakini bado wakulima wamekuwa wakibaki na kiasi kikubwa cha
mahindi na kushindwa kupata masoko hivyo aliiomba Serikali kuiangalia upya
wilaya ya Ludewa kutokana na uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi unaofanyika.
Mgeni rasmi
wa hafla hiyo ya mafunzo ya shamba darasa ambaye ni ofisa kilimo wa wilaya ya
Ludewa Bw.Naftari Mundo akitoa hotuba yake kwa wakulima hao alisema kuwa anatoa
pongezi kwa shirika la ACTN kwa kubuni mafunzo hayo ambayo yatainua uchumi wa
wakulima na Taifa kwa ujumla katika mpango mzima wa uboreshaji wa kilimo
nchini.
Bw.Mundo
alisema kuwa Serikali bado inaangalia uwezekano wa kutafuta mashirika
mbalimbali ya nje ya nchi ili yaweze kuyanunua mazao ya wakulima kwa bei nzuri
hivyo wakulima hawapaswi kukata tama ya kuendelea na kilimo kutokana na kukosa
masoko kwani tayari juhudi za ununuzi wa mazao yao zimeshafanyika.
Aidha
aliwataka wadau mbalimbali wa kilimo kuiga mfano wa ACTN na washirika wake
katika kuendeleza kilimo nchini ili kuweza kuinua pato la taifa na kutengeneza
maisha bora ya wakulima kwani kilimo nio msingi wa maisha ya mtanzania bila
kilimo hakuna chakula.
mwisho
No comments:
Post a Comment