Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba
Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe akiongea na wananchi
Filikunjombe akiupokea mwenge wa Uhuru
Shamba la miti katika kijiji cha Lupanga ambalo lilizinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru
Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya
Vijana wa kundi la sanaa la Ludewa mjini IVA YOUTH GROUP wakipagawisha katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Filikunjombe akisalmiana na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Bw.Juma Khatibu Chum
Mbio za
mwenge wa uhuru zinazoendelea kuzunguka nchi nzima zimeweza kuzindua miradi ya
maendeleo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe yenye thamani zaidi ya shilingi
billion 1.3,miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuzindua zahanati,madarasa na kuweka
mawe ya msingi katika shamba la miti na nyumba ya kulala wageni.
Mbio hizo za
Mwenge ambazo zilikimbizwa katika tarafa ya Mlangali uongozi wa wilaya ya
Ludewa ulizipokea kutoka wilaya ya Njombe kijiji cha Lusitu na ziliweza
kupokelewa kwa shangwe ndelemo na umati wa wakazi wa tarafa hiyo ambapo mkesha
wa mwenye wa Uhuru ulifanyika katika makao makuu ya kata ya Mlangali na baadae
wilaya ya Ludewa uliwakabidhi wilaya ya Wanging’ombe.
Akiupokea
mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya kutoka kwa mkuu wa
wilaya ya Njombe Bi.Salah Dumba alisema kuwa Mwenge wa uhuru ni nuru ya
matumaini kwa watanzania hivyo kila mtanzania anapaswa kuuheshimu na kuuenzi
kutokana na kazi kubwa ya mwenge wa uhuru katika Taifa letu.
Bw.Choya
alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Ludewa wanaimani kubwa na Serikali yao
katika kuwaletea maendeleo na ndio maana walijitokeza kwa wingi katika kuulaki
Mwenge wa Uhuru na umeweza kuzindua miradi mikubwa ambayo imebiniwa na wananchi
kwa kushilikiana na halmashauri ya wilaya ya Ludewa pamoja na Mbunge wa jimbo
la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe.
“Mwenge wa
Uhuru umeweza kuzindua miradi mikubwa ya maendeleo yanye thamani ya shilingi
Bilioni 1 na milioni 350 ambayo imetekelezwa na nguvu za wananchi kwa
kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Ludewa pamoja na Mbunge wa jimbo la
Ludewa hivyo wananchi wanafuraha kubwa kuona miradi yao inazinduliwa na
Mwenge”,alisema Bw.Choya.
Akiongea na
wananchi wa kijiji cha Mangalanyene ambako Mwenge wa uhuru ulizindua Zahanati
Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe alisema kuwaujenzi wa jengo hilo
la Zahanati umegharimu kiasi cha shilingi milioni 40 ikiwa milioni 20 ni
mchango wa nguvu zake na shilingi milioni 20 ni mchango wa nguvu za wananchi na
Halmashauri.
Mh.Filikunjombe
alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Ludewa ni wachapakazi hivyo amekuwa
wakifanya kazi kubwa za kimaendeleo na wamekuwa na furaha kubwa kuona miradi
waliyoifanya kwa nguvu zao inazinduliwa na Mbio za mwenge wa uhuru.
Akifungua
miradi hiyo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2015 Bw.Juma
Khatibu Chum alisema kuwa ujembe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2015 ni Kutumia haki
yako ya kidemokrasia,jiandikishe na kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2015
pia vijana wa leo na ukimwi wazazi tuwajibike,wekeza katika maisha ya
baadae tokomeza maralia.
Bw.Chum alisema kuwa pia ujumbe wa Mwenge wa
uhuru unasema “uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika chukua hatua,kata
mnyororo wa Rushwa chagua kiongozi mzalendo”,hivyo wananchi wanatakiwa kuutumia
ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika uchaguzi uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment