Chama cha
Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
kimeingia katika mgogoro mkubwa kutokana na wanachama wa chama hicho
kushangazwa na kitendo cha uongozi wa chama hicho kutoka kanda ofisi za mkoa wa
Mbeya kufanya uchaguzi wa viongozi wa wilaya kwa kushitukiza.
Wakiongea
kwa nyakazi tofauti baadhi ya wananchama wa chama hicho hapa wilayani kwa
masharti ya kutotajwa majina yao kwa kuhofia kuvuliwa uanachama walisema kuwa
licha ya kuwa uongozi wa awali ulikuwa na mapungufu ya kuwa na migogoro ya mara
kwa mara hasa katika kuendekeza ukabila lakini ulikuwa na watu wenye uwezo wa
kufanya maamuzi kutokana na elimu waliokuwa nayo.
Walisema
kuwa kitendo cha viongozi wa kanda kuitisha mkutano mkuu wa dharula na kufanya
uchaguzi wa viongozi wengine kimewashitua wanachama hao ambao walikuwa na imani
kubwa na viongozi wao wa awali hivyo kuwaletea viongozi wengine ni sawa na
kukivuruga chama na kusababisha kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu ujao.
Aliyekuwa
katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Ludewa
Bw.Kathbet Haule apotakiwa kutolea maelezo kuhusiana na mgogoro huo
unaokitafuna chama alisema kuwa viongozi wa wilaya akiwemo yeye kama katibu
mwenezi hawajavuliwa madaraka na nib ado
wao ni viongozi wa wilaya licha ya kuwa waliochaguliwa kupitia uongozi wa kanda
wanajinadi kuwa wao ndio viongozi.
“sisi ni
viongozi wa chadema wilaya ya Ludewa nabado tunatambulika waliochaguliwa ni
tume tu kama taxforce itakayofanya kazi katika kipindi hiki cha uchaguzi lakini
sisi tutabaki kuwa viongozi wa wilaya na kama wanawatangazia watu kuwa sisi
tumepigwa chini huo ni uongo kwani kazi ya ofisi ya kanda si kuchagua viongozi
wa wilaya”,alisema Bw.Haule.
Kuhusiana na
mgogoro mkubwa unaokitafuna chama hicho wilayani hapa Bw.Haule alisema kuwa ni
kweli baadhi ya viongozi ndani ya chama wamekuwa wakishindwa kuelewana kutokana
na baadhi ya mambo mfano ni katibu na mwenyekiti ndio walikuwa na mgogoro ambao
ungeweza kumalizika kabla ya kufanya uchaguzi uliofanyika.
Bw.Haule
alisema kuwa suala la ukabila ndani ya chama hicho wilayani Ludewa limekuwa
likuzungumzwa mara kwa mara licha ya kuwa hakuna malalamiko kwa maandishi
yaliyowahi wasilishwa katika ofisi yake na katibu ila kumekuwa na minong’ono
kwa baadhi ya wanachama kulalamikia jambo hilo hivyo hakuna uhakika kama jambo
hilo ni chanzo cha migogoro ndani ya chama.
No comments:
Post a Comment