Huyu ndiye Mhandisi Zefania Chaula akiwaaga wajumba baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mjumbe wa NEC wilayani Ludewa
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya akimkabidhi cheti Deo Filikunjombe
Filikunjombe akikabidhiwa cheti
Huyu ndiye mzee Nkwera Hilaly mjumbe wa NEC kwa sasa wilayani Ludewa
wajumbe wa mkutano mkuu Ludewa wakifuatilia mkutano
Mzee Hilaly
Nkwera ambaye ni mwanasiasa mkongwe wilayani Ludewa katika Mkoa Njombe
amemgaragaza vibaya Mhandisi Zefania Chaula katika uchaguzi wa kugombea nafasi
ya halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) NEC kwa kura 43 kwa 11ambazo
alizipata mpinzani wake.
Uchaguzi huo
wa mjumbe wa NEC wilayani Ludewa umefanyika baada ya aliyekuwa mjumbe wa Nec
wilayani hapa Elizabeth Haule kufariki Dunia na wilaya ya Ludewa kukosa
mwakirishi katika Halmashauri kuu ya CCM Taifa.
Akiwashukuru
wajumbe kwa kuibuga mshindi katika uchaguzi huo Mzee Nkwera alisema kuwa
amefurahishwa na kitendo cha wanaccm wilayani Ludewa kuendelea kumwamini katika
utendaji ndani ya Chama cha mapinduzi hivyo atatumia uwezo na akili yake yote
katika kulitumikia taifa na wanaludewa.
Aidha
Mhandisi Chaula alikiri kushindwa vibaya katika uchaguzi huo na kuahidi kuwa
hatagombea nafasi hiyo tena katika maisha yake kwani ni zaidi ya mara moja
amekuwa akigombea nafasi hiyo na kugaragazwa vibaya.
“Nasema haya
kutoka moyoni mimi ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi na nakipenda chama change
hivyo naahidi sitagombea tena katika maisha yangu nafasi hii ya unec kutokana
na ukweli kuwa nahisi siasa inanikataa maana kila nikigombea nashindwa hivyo
ngoja nifanye kazi nyingine pia namtakia kila laheri mzee Nkwera katika
utendaji wake ndani ya chama”,alisema Mhandisi Chaula.
Katika mkutano
huo wa halmashauri kuu ya wilaya ya Ludewa ya Chama cha mapinduzi Mkuu wa
wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya aliweza kumtunuku cheti cha heshima mbunge wa
jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe kwa kushiriki kimamirifu katika mbio za
mwenge wa Uhuru ndani ya mkoa wa Njombe.
Akitoa cheti
hicho Bw.Choya alisema kuwa kutokana na ushiriki alioufanya mh.Filikunjombe
katika mbio cha mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Njombe na ofisi yake wameona
wampatie cheti cha heshima Filikunjombe kwani ni mbunge pekee aliyeshiriki
katika mbio hizo za Mwenge katika mkoa wa Njombe.
Mbunge huyo
wa jimbo la Ludewa Mh.Filikunjombe amekuwa kinara wa kushiriki katika kazi za
maendeleo ndani ya mkoa wa Njombe na katika jimbo lake hivyo alishiriki
kikamirifu katika mbio za Mwenge wa uhuru na hali ambayo iliwafanya wananchi
kujitokeza kwa wingi katika kumuunga mkono Filikunjombe kushiriki mbio za
mwenge wa uhuru.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment