Wananchi wa kata ya Luana wakiwa wamembeba Filikunjombe kutokana na kukubali utendaji wake kazini
wananchi wa kata ya Ludewa Mjini wakiwa wamembeba Filikunjombe wakati akifunga kampeni za kura za maoni
Wananchi wa kata ya Makonde wakimpokea Filikunjombe kwa kumbeba mpaka eneo la mkutano
Filikunjombe akiwaaga wananchi wa kata ya Luana
wananchi wa kata ya Ludewa wakimuingiza Filikunjombe katika kari lake
Filikunjombe akiwaaga wananchi wa kata ya Ludewa
wananchi wa kata ya Mawengi wakimpokea Filikunjombe kwa kumshangilia
Filikunjombe akiwaaga wananchi wa kata ya Ibumi
Vuguvugu la
kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
limeziidi kushika kasi ambapo Mh.Deo Filikunjombe ameendelea kuwafunika
wagombea wenzake vibaya pale anaponadi sera zake kwa wanaccm na kupata mapokezi
makubwa yanayoambatana na kubebwa juu na wananchi pale wanapofunga mikutano ya
kampeni hizo.
Hali hiyo
ambayo imejitokeza katika kata zote lakini siku ya jana katika kata ya Ludewa
mjini hali ya kumshangilia na kumbeba ilizidi kwani umati wa wananchi
uliofulika katika viwanja vya soko kuu la Ludewa mjini ulionekana ukishangilia
na kumbeba juu kwa juu huku wakiimba Deo jembe letu.
Kutokana na hali
hiyo inayotokea kila kata imewafanya wagombea wengine kukata tamaa wagombea hao
ambao ni Kapteni Jacob Mpangala na Mhandisi Zefania Chaula ambao wamekuwa
wakishuhudia matendo hayo yakitokea pale ambapo mwenyekiti wa mkutano
ameshafunga mkutano.
Licha ya
kubebwa na wananchi lakini Filikunjombe amelazimika kuwa mgombea wa mwisho
kujieleza katika mikutano kutokana na wananchi kumsikiliza yeye tu na
kutawanyika akiwa amekwisha jieleza bila kujali kuwa kuna wagombea wengine
ambao wanapaswa kusikilizwa hivyo uongozi wa ccm wilaya umekuwa ukilazimika kumpanga kuwa wa mwisho katika kujinadi.
Azinadi sera
zake katika ukutano wa mwisho ambao ulifanyika kata ya Ludewa Mjini
Filikunjombe alisema kuwa chama cha mapinduzi kina ilani zinazotekelezeka hivyo
wananchi wa wilaya ya Ludewa wanatakiwa kuzingatia mafiga matatu kuanzia rais
ambaye ni Dkt.John Pombe Magufuli wabunge na madiwani.
Filikunjombe
alisema kuwa maendeleo yaliyopatikana kwa muda mfupi wilayani Ludewa ni
kutokana na umakini wa mbunge waliomchagua kupitia chama cha mapinduzi hivyo
wananchi hawapaswi kufanya makosa ya kuchagua vyama vingine kwani Dkt.Magufuli
ni kiongozi makini hakuna asiyejua utendaji wake.
“upendo huu
mnaonionesha mimi kama mbunge wenu ndio mnaotakiwa kumuonesha Dkt.Magufuli
kwani bila yeye hata hizi barabara za lami za mitaa tusingezipata hivyo
nawaomba mnichague mimi pamoja na madiwani wa ccm katika jimbo hili la Ludewa
lakini rais wetu ni Magufuli na nawaomba wananchi wote msipoteze kura hata moja
kwa vyama vingine”,alisema Filikunjombe.
Aidha mmoja
wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Herman Luoga alisema kuwa wananchi wa
jimbo la Ludewa hawana haja ya kuwa na mgombea mwingine wa chama cha mapinduzi kwani
utendaji wa mbunge wao umekuwa ukionekana kwa macho na hata mikoa mingine
inaujua utendaji wa Filikunjombe.
Bw.Luoga aliwataka
wananchi wengine kutohangaika na vyama vya upinzani wakati mbunge wao anafanya
kazi waliyomtuma awapo bungeni kwani kwa kujiunga na upinzani ni sawa na
kusaliti kazi za kimaendeleo ambazo Filikunjombe amekuwa mstari wa mbele
kuzitetea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment