Chama cha
Demokrasia na Maendeleo wilayani Ludewa kimeendeleana na mtifuano mkali katika
kumsaka mgombea mmoja wa ubunge wilayani hapa ambapo kila mgombea amekuwa
akipita huku na kule kusaka kura kwa wajumbe wa hama hicho huku baadhi yao
wakituhumiana kutumia pesa zaidi.
Akiongea na
waandishi wa habari jioni ya leo Wakili Paulo Kalomo ambaye ni miongoni mwa
wagombea wa nafasi hiyo akitokea mwambao wa ziwa Nyasa alisema kuwa mpaka sasa
kuma wagombea wanne hivyo yeye amekuwa na mvuto zaidi kwa wajumbe hali ambayo
inawafanya wagombea wenzake kukata tamaa na kuwarubuni wajumbe.
Wakili
Kalomo alisema kuwa akifanikiwa kuchukua nafasi hiyo atakibadirisha chama cha
demokrasia na maendeleo wilayani Ludewa kwa kujijenga kuanzia vijijini hadi
ngazi ya wilaya hivyo amewataka wajumbe wa chama hicho kutorubuniwa na baadhi
ya wagombea katika kura za maoni zinazotarajiwa kupigwa kesho tarehe 23/7/2015
katika makao makuu ya wilaya kwani yeye anamipango endelevu kwa wilaya ya
Ludewa.
No comments:
Post a Comment