waha ndio wagombea ubungea jimbo la Ludewa kwa tiketi ya CCM wakiwasalimia wananchi
Kutoka kulia anayeandika ni Mhandisi Zefania Chaula,katikati ni Kampen Jacob Mpangala na kushoto mwenye jaketi ni Deo Filikunjombe
wananchi wa kata ya Lugarawa wakianza kutawanyika baada ya Filikunjombe kumaliza kuongea
wananchi wakitawanyika mkutanoni na kuelekea makwao na kuwaacha wagombea wengine wakiwa bado hawaja jieleza
WANANCHI
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameanza kuwaadhibu wagombe wanaowania
nafasi ya Ubunge na wanaompinga Filikunjombe kwa kuwaacha peke yao katika
viwanja vya mikutano pale anapomaliza kujieleza Deo Filikunjombe na kujibu
maswali ya wananchi wanapohitaji ufafanuzi.
Hali hiyo
imeanza kujitokeza juzi katika kata ya Ludende,Milo na Lugarawa katika mikutano
inayoitishwa na chama cha mapinduzi ili kuwanadi wagombea watatu wa chama hicho
kwa wanachama ili kuweza kupiga kura za maoni ambazo zitampitisha mgombea mmoja
wa ccm ambaye atapambana na wagombea wa vyama pinzani.
Katika jimbo
la Ludewa ndani ya chama cha mapinduzi wamejitokeza wagombea wawili wakipambana
na mgombea aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo wagombea hao ni Mhandisi Zefania
Chaula,Kapten Jacob Mpangala na Deo Filikunjombe ambapo hali imekuwa mbaya
zaidi kwa wapinzani wa Filikunjombe kwani anapopangwa kuanza kujieleza
Filikunjombe wagombea wengine hubaki bila watu na kujikuta wakibaki wao na
viongozi wa ccm wilaya.
Mmoja wa
wananchi ambao walitoka katika mkutano wa hadhara katika kata ya Lugarawa baada
ya Filikunjombe kumaliza kujinadi kwa wananchi Bw.Yusto Mgimba alisema kuwa
wananchi wamekuwa na shauku ya kumsikiliza Filikunjombe na wamekuwa na imani
naye hivyo hawana mpango wa kuwasikiliza wengine kwani hawajulikani kwa
wananchi.
Bw.Mgimba
alisema kuwa Filikunjombe bado anakubalika na wananchi wa wilaya ya Ludewa
kwani maendeleo na ahadi alizoziahidi mwaka 2010 amezitekeleza pia wanafuatilia
kazi anazozifanya awapo Bungeni za kuwatetea wananchi wake hivyo hakuna sababu
ya kubadirisha mbunge kama miaka mingine.
“tunawashangaa
wagombea hawa wengine wanavyotueleza watafuatilia miradi ya chuma cha Liganga
na makaa yam awe ya Nchuchuma na ujenzi wa viwanda vyake wakati kwa macho yetu
tumemuona na tumemsikia akifunga Bunge
rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete akisema kuwa mwaka huu atakuja kuweka
mawe ya msingi ya ujenzi wa viwanda hivyo sasa wao watafuatilia wapi wakati
kazi hiyo sisi wananchi tulimtuma Filikunjombe na majibu tumeyapata?”,alisema
Bw.Mgimba.
Bw.Mgimba
alisema kuwa wananchi hawaoni sababu ya kuendelea kuwasikiliza hao wengine
wasiowajua hivyo wakishamsikiliza mbunge wao ambao wanamkubali jembe lao
wanatawanyika kwani wanajua watadanganywa tu na hawa wengine kutokana na ukweli
kwamba hawana jipya la kuwafanyia wananchi.
Aidha
msimamizi wa mchakato huo wa kumpata mgombea mmoja wa chama cha mapinduzi
ambaye ni Mnec wa wialaya ya Ludewa mzee Hilaly Nkwera alisema kuwa mchakato
unakwenda vizuri na hauna kasoro kwani wagombea wote wametulia na itabidi
wakubali matokea hata kama baadhi hawakubaliki na wananchi.
Kuhusu
wananchi kuondoka katika mikutano baada ya Filikunjombe kumaliza kijieleza Mzee
Nkwera alisema kuwa suala hilo lipo na inashindikana kuwazuia richa ya kuwa wasimamizi
wamekuwa wakitoa angalizo kwa wananchi kutoa ondoka lakini imekuwa shida hivyo
imebidi wagombea wote wakubadliane kila mkutano Deo Filikunjombe awe wa mwisho
kujieleza ili kuepusha hali hiyo.
Mzee Nkwera
alisema kuwa makubaliano hayo yanaweza kusaidia kwa upande Fulani ili wagombea
wengine wapate kusikilizwa sera zao kwa wananchi kwani bila kufanya hivyo hali
itakuwa ni ile ile ya awali ya wananchi kutawanyika baada ya kumsikiliza
Filikunjombe na kuwaacha wagombea wengine bila wasikilizaji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment