Bw.Mwapinga mwenye fulana ya rangi ya Kijani akimkabidhi mipira mwenyekiti wa kijiji cha Shaurimoyo Bw.Mwinuka
Bw.Mwapinga akimkabidhi jezi mwenyekiti wa kijiji cha Shaurimoyo Bw.Adriano Mwinuka
Bw.Mwapinga akimkabidhi saruji mwenyekiti wa kijiji cha Shaurimoyo Bw.Mwinuka
Bw.Mwapinga akipongezwa na mabalozi wa Shaurimoyo
hawa ndio mabalozi wa kijiji cha Shaurimoyo kata ya Lugarawa wilayani Ludewa
hili ndilo jengo la shule ya msingi shaurimoyo ambalo wafadhiri mbalimbali wanalichangia ukarabati wake
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya mkoa wa Njombe na
mchumi wa kata ya Lugarawa kupitia chama cha Mapinduzi Bw.Damian Mwapinga
amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi katika ngazi ya vitongoji,vijiji hadi
kata kuhimiza uletaji maendeleo kwa wananchi bila kujari itikadi ya vyama vya
siasa.
Bw.Mwapinga aliyasema hayo jana katika kijiji cha
Shaurimoyo kata ya Lugarawa wilayani Ludewa wakati akiongea na mabalozi wa
nyumba kumi ambapo aliweza kutoa vifaa vya ujenzi ambavyo ni saruji mifuko kumi
na nondo rolu nne vyote vikiwa na thamani ya shilingi 340000% pia alitoa vitaa
vya michezo ambavyo ni jezi seti moja na mpira mmoja kwa timu ya mpira wa miguu
Shaurimoyo.
Alisema kuwa wananchi wanahitaji maendeleo na sio
malumbano ya kisiasa hivyo yeye kama kada wa chama cha mapinduzi ameona umuhimu
wa kuleta maendeleo kwa wananchi ni pamoja na kupunguza umaskini hivyo aliuomba
uongozi wa kijiji kutumia nondo na saruji hiyo katika ukarabati wa shule ya
msingi shaurimoyo.
Bw.Mwapinga aliwataka viongozi wa vitongoji,
mashina na vijiji kuungana na wananchi ili kufanikisha suala zima la maisha
bora kwa wananchi kwani kumekuwa na shida kubwa inayosdababishwa na baadhi ya
vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikiwashauri wananchi kutofanya kazi za
kimaendeleo kwa kusema maendeleo yataletwa na Serikali.
"nawaomba viongozi wenzangu kushiriki katika
uletaji wa maendeleo kwa wananchi ambao wanakiu ya maendeleo na sio siasa
ambazo zianarudisha nyuma maendeleo na hivi vifa ninavyovitoa nawaomba kama
viongozi wenzangu kuvisimamia vifaa hivi ili vitumike kwa malengo
yaliyokusudiwa na wananchi waone mazuri ya Serikali yao inayoongozwa na
ccm",alisema Bw.Mwapinga.
Akipokea vifaa hivyo mwenyekiti wa kijiji cha
Shaurimoyo Bw.Adriano Mwinuka amesema kuwa jamii ya Shaurimoyo imevipokea vifaa
hivyo kwa mikono miwili kutokana na wananchi hao kuchangishana fedha za
kununulia saruji na nondo kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo gharama za
manunuzi zitapungua kutokana na mjumbe huyo kuchangia sehemu ya vifaa hivyo.
Bw.Mwinuka amesema kuwa vifaa hivyo vitatumika kwa ukarabati wa
majengo ya madarasa ambayo yalijengwa kwa muda mrefu na mbao za majengo hayo
zimeliwa na mchwa ambazo zinaweza kuleta madhara kwa wanafunzi hasa msimu wa
mvua unapowadia.
Aliwataka wadau mbalimbali kuendelea kuchangia
ujenzi wa shule hiyo ambayo imekuwa ikihitaji ukarabati kwa muda mrefu bila
mafanikio kutokana na michango ya wananchi kutotoshereza katika ununuzi wa
vifaa vinavyohitajika hivyo kama watatokea wadau kama Bw.Mwapinga itakuwa ni
vizuri na italeta tija kwa wananchi.
mwisho.
No comments:
Post a Comment