Haya ndio maporomoko ya mto Lupali katika kijiji cha Njelela wilayani Ludewa yanayotarajia kuzalisha umeme utakao nufaisha vijiji 19
Viongozi wa shirika la LCBA na wataalamu wa upimaji wa Ardhi ili kupima eneo la kufunga mitambo
Wajumbe wa shirika la LCBA wakiangalia ukubwa wa maporomoko ya mto Lupali
Mwandishi wa mtandao huu Nickson Mahundi akiwa na Bahati katika maporomoko ya mto Lupali katika kijiji cha Njelela
Wataalamu wakiendelea na upimaji katika eneo la mradi wa umeme
Wataalamu wipima umbali kutoka mtoni
Mjumbe wa LCBA Bw.Donoto Mgeni maarufu kwa jina la Ndicheliwe akisaidia kusafisha mazingira kwaajili ya upimaji
Katibu wa shirika la LCBA Bw.Joseph Kayombo akiweka alama eneo la mradi
maji ya mto Lupali
Alama zikiendelea kuwekwa
msitu unaotililisha maji katika mto Lupali
mambo ya vipimo yakiendelea mto Lupali
msitu wa mto Lupali
Mwandishi wa mtandao huu akiwa katika maporomoko ya mto Lupali
Wananchi waVijiji 19 wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe
wanatarajia kunufaika na huduma ya umeme utakao zalishwa na shirika lisilo la
Serikali linalojihusisha na mambo mbalimbali ya kijamii la Ludewa Capacity
Bulding Association(LCBA) lenye makao yake makuu Ludewa mjini.
Akiongea na waandishi wa habari katibu wa shirika hilo
Bw.Joseph Kayombo alisema shirika lake linatarajia kuuzalisha umeme huo kupitia
maporomoko ya Mto Lupali ulioko katika kijiji cha Njelela kata ya Mundindi
wilayani Ludewa.
Bw.Kayombo alisema umeme huo unakadiliwa kutoa megawalt 30
ambazo zitavinufaisha vijiji 19 kwa gharama nafuu kutokana na shirika hilo
kujihusisha na utoaji misaada na elimu katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya
ya Ludewa.
Alivitaja vijiji vitakavyonufaika na huduma hiyo katika kata
ya Mundindi kijiji cha Mundindi,Amani na Njelela,kata ya Ibumi ni kjiji cha
Ibumi na Nyamalamba kata ya Madilu ni kijiji cha Madilu,Ilininda,Ilawa,Mfalasi
na Manga kata ya Madope kijiji cha Madope,Luvuyo,Lusitu na Mangalanyene.
Vijiji vingine ni Mkongobaki,Lipangala,Ugela,Shaurimoyo na
Mdilidili hata hivyo alisema umeme huo utakuwa na nguvu kubwa hivyo unaweza
kusambaa katika vijiji vingi zaidi itakavyowezekana kutokana na wafadhiri wa
mradi huo watakavyopendekeza.
“Tumeshafuata hatua zote za kisheria na REA wanatutambua
hivyo wananchi wanapaswa kujenga nyumba nzuri za kudumu ili wajiandae na ujio
wa neema hivyo ya umeme kwa kunavijiji tokea nchi hii ipate uhuru havijawahi
sikia kama vinaweza kupata umeme hivyo wananchi watupe ushirikiano”,alisema
Bw.Kayombo.
Diwani wa kata ya Mundindi kupitia chama cha Mapinduzi ambako
umeme huo utazalishwa Bw.Vicent Mgina alisema amefurahishwa na jambo hilo kutokana
na ukweli kwamba umeme ndio chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali
Duniani.
Bw.Mgina alisema wananchi wake kupitia umeme watapata fulsa
ya kufanya biashara mbalimbali na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kujipatia
kipato kwa umeme huo utaenda sambamba na ujenzi wa chuo cha VETA katika kijiji
cha Shaurimoyo hivyo watakaosoma chuo hicho wataweza kujiajiri kwa kuanzisha
karakana zao.
Alisema kitu cha msingi kwa shirika hilo ni kufuata sheria za
nchi na kuwashirikisha wananchi ili waweze kuona wao ni wenye mradi huo ili
kuondoa migongano inayoweza kujitokeza kutokana na tamaduni za wananchi wa
maeneo hayo kulima mabondeni katika vyanzo vya maji.
Aidha mjumbe wa shirika la LCBA Bw.Lazaro Mwinuka alifafanua
kuwa shirika hilo unakadiliwakutumia kiasi cha shilingi 40 Bilion kutoka Bank ya
Dunia kupitia REA ambazo zitafanya kazi zote mpaka mradi huo utakapo kamilika.
Bw.Mwinuka alisema mchakato wa mradi huo umeshaanza lakini
unatarajia kumamilika ifikapo mwaka 2014 kutokana na ukubwa wa mradi hivyo
wananchi wa vijiji tajwa wanatakiwa kuanza maandalizi katika nyumba zao ili
waweze kunufaika na mradi huo.
Hata hivyo Bw.Donota Mgeni maarufu kwa jina la Ndicheliwe
mfanyabiashara wilayani Ludewa na mjumbe wa LCBA alisema wananchi wenye
shughuri zao eneo la mradi watalipwa fidia zao mapema mwaka huu ili kupisha
mradi huo.
Bw.Mgeni alisema kinachotakiwa kwa wananchi ni kutoa
ushirikiano kwa viongozi wa vijiji na kata husika wanashirikishwa kwa kila
jambo ili waweze kutambua manufaa ya umeme huo katika vijiji na kata zao na si
vinginevyo.
Aliwataka kutokuwa na wasiwasi na shirka lao kutokana na
wananchi hao kudanganywa na mashirka mengi yaliyowahi fika katika mapolomoko
hayo na kuahidi yataweka umeme lakini hayakutimiza ahadi hizo na kutokomea
kusikojulikana.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment