Na Ibrahim
Yassin,Kyela
ZAIDI
ya tani 20 za dagaa nyasa kutoka wilaya
ya Ludewa mkoani Njombe zimezuiliwa kwenye bandari ya Itungi iliyopo wilayani
Kyela mkoani Mbeya zilizokuwa zikisafirishwa kwenda kuuzwa mikoani kupitia bandari hiyo.
Hatua hiyo
ya kuzuiliwa kwa dagaa hizo kumetokana na hatua ya Serikali wilayani Kyela
chini ya mkuu wa wilaya Magret Marenga,kufuatia kuzuka hofu kuwa kuna mgodi wa
machimbo nchini Malawi kuvujisha maji machafu yanayodaiwa kuwa na sumu hivyo
kuwa na hofu ya kupata madhara pindi walapo samaki hizo.
Kufuatia
hofu hiyo Serikali mkoani Mbeya ililifunga soko la Samaki wilayani humo pamoja
na kuwazuia wavuvi wasivue samaki hadi pale uchunguzi wa mkemia mkuu wa
Serikali aliyechukua sampuli ya samaki hizo kwa ajili ya kuzipima na wataruhusu
shughuri za uvuvi na uuzwaji wa samaki pindi majibu ya mkemia yatakapo tolewa.
Ikiwa hali
hiyo ipo hivyo zaidi ya wavuvi na wafanyabiashara kumi kutoka wilayani Ludewa
waliokuwa wakisafirisha dagaa hizo dagaa zao zimezuiliwa katika bandari hiyo
hadi pale majibu ya mkemia yatakapotolewa kama zina sumu au laa.
Kufuati
Serikali mkoani Mbeya kuzuia zoezi hilo lakini bado agizo hilo linaonekana
kupuuzwa baada ya shughuri za uvuvi kuendelea huku wauzaji wa samaki
wakitembeza mitaani bila kificho ambapo wafanyabiashara kutoka Ludewa wakizidi
kusota Gest wakisubili majibu ya Mkemia mkuu.
Franko
Ngoye,Titto Kayombo na Kevin Haule ni miungoni mwa waliozuiliwa kusafirisha
dagaa katika Bandari hiyo walisema wao hawana taarifa ya uwepo wa agizo hilo na
kuwa katika wilaya yao Tarafa yote ya Mwambao wanatumia maji ya ziwa hilo kwa
shughuri zote ikiwemo kunywa toka enzi za mababu zao.
Walisema walipofika
na dagaa hizo tarehe 18 mwezi huu katika Bandari hiyo lengo lao ni kusafirisha
kwenda mikoani kwa ajili ya kuziuza lakini samaki hizo zilizuiliwa kusafiriswa
wakidai kuna hofu ya samaki hizo kuwa na sumu na kuwa hawakuambiwa wasubiri
hadi lini.
Walisema hivi
sasa wameishiwa pesa za matumizi na za kulipa Gest na kufikia hatua ya kula mlo
mmoja kwa siku na kurudishwa vyumba na kulundikana katika chumba kumoja
kutokana na ukosefu wa fedha huku hatma yao kutojulikani.
Waliongeza kuwa
Serikali wilayani Kyela imekuwa ikiwanyanyasa miaka mingi pindi wasafirishapo
samaki kupitia Bandari hiyo kwa kuwatoza pesa nyingi pamoja na kuwa wanakuwa
wanalipia katika wilaya yao na kwamba hulipia Shiling 500 hadi 400 kwa boksi
lakini wakija kyela wanaambiwa walipie upya.
Akijibu hoja
hizo mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema ni kweli Serikali imezuiwa kwa
muda kuuza samaki pamoja na wavuvi kuendelea kuvua kwa hofu hiyo ya kuwa ziwa
nyasa kuwa na sumu hadi pale majibu ya mkemia mkuu wa Serikali atakapo leta
majibu baada ya kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.
Aliongeza kuwa
wavuvi hao wavute subira hadi juma tatu kesho majibu yatakuwa tayari,na kwamba
kama itaonekana dagaa hao wanansumu watafukiwa shimoni na kama itathibitika
kutokuwa na sumu wataruhusu shughuri hizo kuendelea.
Kuhusu wavuvi
kukaidi agizo hilo kwa kuendelea kuvua huku wafanyabiashara kuuza samaki hao
mitaani alisema inatokana na uongozi wa Serikali wilayani humo kutosimamia
ipasavyo zoezi hilo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment