Wananchi wa kata ya Lugarawa wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe jana waligoma kwa muda wa masaa 3 kuuzika mwili wa kijana January Mtitu ambaye alipigwa risasi na askari wa jeshi la pilisi Abduel Hamza Nyuki G 6352 D/C wakishinikiza gharama za awali za mazishi zilizogharimiwa na ndugu wa marehemu zilipwe na Jeshi la polisi ndipo mazishi yafanyike.
Licha ya kuwa viongozi wa kiwilaya ambao ni kamati ya ulizi na usalama wilaya ya Ludewa wakiongozwa na mwenyekiti wao ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha kuwashawishi kuacha mgomo huo lakini hali ilizidi kuwa mbaya mpaka madai yao yalipo timizwa ndipo wakakubali kumzika kijana huyo.
Tukio la kuuawa kwa kijana huyo
limetokea baada ya Askari Abduel kutoroka lindo katika bank ya NMB wilayani hapa usiku wa kuamkia tarehe 23/01/2015 na kwenda nyumbani kwa marehemu maeneo
ya Ludewa mjini mtaa wa Mdonga usiku wa saa sita na kufanya uharifu huo hali
ambayo imewashtua wananchi wa mji wa Ludewa ambao hawajawahi kuona matukio kama
hayo yakifanyika katika mji wao na kutaka kufanya maandamano kabla ya kuzuiwa na uongozi wa wilaya.
Bado mpaka sasa sababu kubwa ya kuuawa kijano huyo hazijatolewa rasmi hivyo upelelezi bado unaendelea ili kujua chanzo cha mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment