Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

January 28, 2015

TAMASHA LA FUNGA MWAKA 2014 NA BEST FM LILIVYOFANA WILAYANI LUDEWA.

 umati wa watu katika tamasha hilo




 meneja wa best fm Bi.Deograsia Nyoni akiongea na wadau
hii ndio safu ya wafanyakazi wa Best fm radio
Mwanahabari mwandamizi wilayani Ludewa Bw.Bazil Makungu akiongea na wadau
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.William Waziri akihutubia
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akiongea na umati wa watu waliofulika katika tamasha hilo kulia ni Meneja wa radio best fm Bi.Deograsia Nyoni
Seleman Chikuti toka Iva youth group wakipagawisha mashabiki


Msanii wa kikundi cha Iva youth group Seleman Chikuti akipagawisha jukwaa


Tamasha la funga mwaka wa 2014 na Radio best fm iliyoko wilayani Ludewa limeonesha mabadiriko makubwa kwa wanaludewa tofauti na matamasha mengine yaliyowahi fanyika wilayani hapa hasa kwa wasanii wazawa.


Akiongea wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo meneja wa kituo cha radio cha Besf fm Bi.Deograsia Nyoni alisema lengo la tamasha hilo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wanaoshikiliza matangazo ya kituo hicho cha radio kinachorusha matangazo yake kupitia masafa ya 90.5 katika wilaya ya Ludewa.


Bi.Nyoni alisema kituo hicho cha radio kimekuwa ukombozi mkubwa kwa analudewa na wilaya nyingine zilizoko pembezoni mwa Ziwa Nyasa kwani awali wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakisikiliza taarifa za radeio za nchi jirani ya Malawi.


Alisema kikubwa ni kupata ushirikiano wakutosha kutoka kwa wadau mbalimbali ukiwemo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ili kuendelea kuwapatia taarifa na burudani wananchi wa wilaya ya Ludewa na wilaya za Mkoa wa Ruvuma na Mbeya ambako radio hiyo inasikika vizuri.


“Tamasha hili linalengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine watafahamiana hasa watuma salamu pia tunaomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwani ushirikiano tulio nao bado haurizishi”,Alisema Bi.Nyoni.


Akitoa hotuba kwa wadau mbalimbali mgeni rasmi wa tamasha hilo ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.William Waziri alisema radio hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wilaya ya Ludewa hivyo alimpongeza mkurugenzi mkuu wa kituo hicho cha radio kwa kuwa na mawazo mazuri ya kuanzisha kituo hicho.


Bw.Waziri alisema halmashauri ya wilaya itahakikisha inakuwa na ushirikiano wa kutosha na kituo hicho cha radio ili kumtia moyo mmiliki hivyo alimuomba mmiliki kama ataweza kuanzisha kituo cha television ili wananchi waweze kupata taarifa zaidi.


Mwisho.

No comments: